Viongozi wataka shughuli ya kubinafsisha sekta ya sukari nchini kusitishwa mara moja
15th September, 2015
Viongozi wa kisiasa kutoka maeneo yanakokuza miwa wametaka shughuli ya kubinafsisha sekta ya sukari nchini kusitishwa mara moja na kuanzishwa upya. Viongozi hao wamesema washikadau wakuu hawajahusishwa katika shughuli ilhali inagusia baadhi ya maswala nyeti mathalan ardhi za upanzi wa miwa. Viongozi hao wakiwemo Magavana watano, wabunge na Maseneta wamesema hayo walipokongamana mjini Mombasa kwenye kikao na tume ya ubinafsishaji nchini