Mwana Muziki Charles Jaguar atishia kujiuzulu kutoka NACADA
29th June, 2015
Mwanamuziki charles njagua kanyi ambaye anafahamika kama jaguar ametishia kujiuzulu kama mwanachama wa bodi ya NACADA, mwanamuziki huyo aliyechaguliwa kama mwanachama katika bodi hiyo na rais uhuru kenyatta miezi miwli iliyopita amedokeza kuwa ufisadi umekithiri katika bodi hiyo. Shirika hilo limehusika katika mivutano kumhusu mwenyekiti john mututho na kundi la wanachama wa bodi. Sasa jaguar anataka uchunguzi kufanywa kwa wiki mbili au ajiuzulu.