COTU yapinga pendekezo la KEPSA kuhusu malipo ya wafanyikazi
6th April, 2015
Pendekezo lililotolewa na muungano wa sekta ya kibinafsi, KEPSA kuhusu malipo ya wafanyikazi kwamba yatolewe kulingana na mchango wanaoutoa kwa shirika husika badala ya kuzingatia muda alioutumia mfanyikazi huyo akiwa kazini, limekosolewa vikali na katibu mkuu wa chama cha COTU Francis Atwoli.