Walimu walipwa mshahara wa siku kumi pekee
2nd August, 2013
Walimu wa shule za msingi wamepokea mishahara ya siku kumi pekee za mwezi wa julai; huku wenzao wa shule za sekondari wakipokea mshahara wote. Kumaanisha tume ya huduma kwa walimu-tsc imetimiza ilivyoahidi kutowaalipa walimu kwa kushiriki mgomoni kinyume cha sheria. Mwanahabari frank otieno anaripoti kwamba hatua hii bila shaka inafungua ukurasa mwingine wa malumbano baina ya chama cha knut na serikali, na sasa ilani ya siku saba iliyotolewa ya mgomo mwingine inaonekana kuelekea ukiongoni juma nne ijayo.