News : Wanariadha wakaguliwa kama wanatumia dawa za kusisimua misuli
10th December, 2012
Shirika la riadha nchini AK, limesisitiza kwamba liko tayari kupigana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli zilizoharamishwa kutumiwa na wanariadha wa Kenya. Mwenyekiti Isaiah Kilpagat alisema leo kwamba shirika hilo limeikabidhi serikali stakabadhi zenye madai kuwa baadhi ya wanariadha wa Kenya wanatumia tembe za kuongezea nguvu mwilini.