1st April, 2022
Maafisa wa usalama katika kaunti ya Machakos wanamtafuta jamaa mmoja kuhusiana na mauaji ya mkewe saa za usiku wa manane.
Faith Mueni Mutinda mwenye umri wa miaka 35 kutoka eneo la kikumbo kaunti ndogo ya Kalama adaiwa alienda kulala kama kawaida baada ya mlo pamoja na mumewe Harrison Mutisya ila hakuamka.
Alipatikana na majeraha ya panga kichwani kwenye mkono wake huku mwili wake ukiwa umeloa damu.