Zile vitu wanagomea ni vitu hazimake sense. Hawagomi eti juu shule haina walimu wa kutosha, ama kwa sababu hawana vitabu za kustudy nazo, unapata wanagomea chakula. Photo: The Standard

Kuna maswali mengi sana mimi ninajiuliza. Nini inaendelea mashuleni? Ni wanafunzi wamekuwa wajinga ama ni nini noma nao? Unapata wanafunzi wanafukuzwa shule waende  kuleta School fees nyumbani na kumbe mtoi alishalipiwa fees last term. Yaani amemanga pesa za mzazi bila kulipa kwa shule.

Mwanafunzi anakula fees na wanafunzi wenzake eti hakupewa pocket money ya kutosha. Shuleni mnapewa chakula, kuna dorm za kulala, pocket money mingi unayodai kama mwanafunzi ni ya nini?

Kitu inanijamishanga ni vile unapata hii shule wakigoma leo, shule zingine zinafuata njia hio hio ya kugoma. Na zile vitu wanagomea ni vitu hazimake sense. Hawagomi eti juu shule haina walimu wa kutosha, ama kwa sababu hawana vitabu za kustudy nazo, unapata wanagomea chakula. Mara eti wamekula githeri sana na menu haibadilishwi. Then wanademand eti wapikiangwe hata chapati, mpaka unashindwa wanafunzi elfu tano utawezaje kuwapikia chapati mbili mbili. Nani atawapikia chapati elfu kumi kila wednesday.

Kumbuka hamukuenda shule kukula, mlienda kusoma vitabu. Juzi karibu shule tano zimesetiwa nare na wanafunzi. Mbona mchome shule mahali unasomea, hata kama nikugoma gomeni lakini msichome shule juu ni mzazi wenu ama ndio unapeleka hasara.

Walimu wakigoma hawachomangi shule, mbona nyinyi watoi ndio mchome. Hata wabunge wanademostrate mpaka wanalala kwa barabara lakini hawajawahi choma bunge. Wanafunzi mtawacha ujinga ya kuchoma mashule.

Undeni baro ya Syokimau

Juzi nilikua syokimau, na kwa bahati mbaya ama nzuri nikapitia Kiungani road. Nakwambia  hiyo barabara ni kama shamba. Kidogo nikapita baze ya watu wa nduthi wakaniona na wakaanza kunituma wakitaka niambie MCA, mbunge,senator, governor na wale wote wanahusika na kujenga barabara huko machakos county, watengenezee masafara hio road.

 Ndio maana leo nikaamua story za mtaa ni Kiungani road syokimau,niliwahoji hoji na wakanitembeza kwa barabara zingine za kuingia Syokimau nikatapa kweli zimewekwa lami. Viongozi wasaidie wasee