Please enable JavaScript to read this content.
Hivi sasa imebainika kwamba katika jimbo la Karnataka nchini India kunaishi jamii almaarufu kama Siddis ambao ni vizazi wa Waafrika watumwa walioachwa msitu mmoja ufuoni mwa bahari hindi wakati utumwa ulipositishwa mwaka 1848.
Mnamo miaka ya mwishoni mwa biashara ya utumwa, wanahistoria wanajitokeza kusema kwamba kinara mmoja wa jeshi la Warabu aliyekuwa akiongoza msafara wa watumwa kwa jina Muhammad bin Qasim alikuwa wa kwanza kuingiza msafara katika ufuo wa bandari ya Bharuch, eneo la Gujarat karibu miaka ya 628 AD hadi 712 AD.
Msafara wa jamii hii ya vizazi vya Waafrika (Siddis), wengi walitokea Afrika mashariki hususan Kenya na Ethiopia. Ingawa hivyo, Ushahidi mwingi unaotafakariwa kutokana na mila na desturi ya jamii hii kule India, yashikana sawa na zile za mwambao wa pwani ya Kenya.
Wengi wa wale ambao wamewahi kuwatembelea Siddis wa India, wakiwa ni pamoja na wandishi wa habari na jinsi wanavyozungumza na kuonyesha matamanio yao barani Afrika, kumeonyesha dhahiri kuwa wengi wa jamii hii ya Siddis wametokea Kenya.
Mtaalam mmoja wa masuala ya kijamii na makabila Dkt. Snehalata Shetty kwenye ripoti ya utafi ti wake kuhusiana na ujio wa Siddis katika sehemu ya Karnataka nchini India, anasema kweli hawa ni vizazi wa Waafrika ambao waliwasili kupitia njia ya bahari na vizazi vyao vyajumuisha nchi kama vile Kenya, Burundi, DRC, Rwanda na Uganda.
Historia yao vile vile yawaweka wazi kuwa Siddis walitupwa nchini India karne za 16 na 19 (16th na 19th Century) wakiwa watumwa chini ya mikono ya Wazungu Wareno na Waholanzi (Slaves by the Dutch and Portuguese).
Dkt. Shetty anazungumzia mfano maalum unaopatikana kwenye kumbukumbu ya merikebu (meli ama mashua) iliyotoa nanga kutoka Uingereza kuelekea Magharib mwa pwani ya India mnamo mwaka 1832 ambapo inaelezea msafara wa Waingereza saba (7) wasimamizi, wahandisi waingereza sita (6), na Siddis kumi na watano (15) ambao kazi yao ilikuwa kuchochea kuni za kuendesha meli hiyo.
Maisha ya udhalimu Jamii ya Siddis ambao wengine wanasema wanaweza kuwa Wagiriama (Kenya), Wanyamwezi (Tanzania) ama Buganda (Uganda) wanakabiliwa na maisha magumu ya msituni na ubaguzi wa rangi sawa na jinsi Waafrika wa Afrika Kusini walivyoishi kwa miaka mingi kwa kubaguliwa.
Mbali na wachache wao ambao wamefanikiwa kusoma na kupata kazi chache serikalini, wengi wao leo hii watamani kutambua ni vizazi wa kutoka wapi barani Afrika waweze kuregea nyumbani.
Jina lao la Siddis, wadadisi wengine wanasema linapatikana sana katika jamii ya pwani ya Kenya, katika jamii ya Wagiriama ambao wanayo majina ya Sidi kwenye ukoo wao.
Kwa miango ya miaka yote hii, vizazi vyote vya jamii ya Siddis (Waafrika) waliotupwa msitu wa Karnataka nchini India, wameishi kwa machungu, taabu na mashaka ya udhalimu wa kibinaadamu.
Kabila hili awali limekuwa linaishi sawa kama Wanyama huku Wahindi asilia wa India wakiwapuuza tu kama Wanyama mwitu.
Habari za uhai wao nchini India, zimejitokeza juzi juzi tu ambapo jamaa wengi kutoka barani afrika na ulaya wametia bidi kuwatembelea kujionea wenyewe na kupata fursa ya kupata historia yao zaidi kuhusiana na damu za vizazi vyao vya afrika.
Kwa miaka, wametengwa inchini India kutokana na asilia yao ya rangi, historia yao kwamba ni waja wa watumwa waliotupwa hapo kuanza maisha ama kuangamia.
Stay informed. Subscribe to our newsletter
Maumbile yao kamili ya kiafrika, nywele na tamaduni zao zimewalenga kudhulumiwa kama wageni wa bara hilo la Wahindi.
Kulingana na shirika lenye kuangazia maslahi yao la Uttara Kannada District Social Welfare, linasema kuwa jamii hii ya Siddis, imekuwa itegemea mazao ya msituni kujikimu kiuchumi na kujitegemea kimaisha kutokana kwamba wametengwa kuwa ni jamii isiyotakikana nchini humo.
Yaaminika miundo msingi maeneo yao ni ya kusikitisha na ni juzi tu, yapata miaka kumi iliyopita ndio wengi wao wameanza kuwapeleka watoto wao shule.
Mazulia ya matajiri
Sawa na jamii nyingine maskini za Kenya na barani afrika, Siddis vile vile hukumbukwa na Wahindi wakati wa kura, ikiwa kuna uchaguzi mkuu ambapo wanasiasa wako tayari kuwakodishia matingatinga kuja kuwa beba na kuwanunulia mkate na soda kama ilivyo nchi nyingi baina ya maskini na matajiri wanasiasa.
Taifa la India pia limewatambua wakati wa haja ya kitaifa. Hii inadhihirishwa wakati mmoja ambapo raia wao kutoka kwa jamii hii ya Siddis, aliwashindia dhahabu kwenye mbio za riadha na kuwapatia sifa ulimwenguni.
Mbali na michezo fulani na kura, jamii hii hutupiliwa mbali kama Wanyama wa kawaida. Kulingana na sensa ya India, Waafrika hawa WALIOTUPWA MSITU INDIA SASA WATAMANI KURUDI Jamaa wa jamii ya Siddis akiwa na mtoto wake wadhulumiwa nchini India kwa kuwa ni vizazi vya watumwa kutoka Kenya.
Msichana wa jamii ya Siddis vizazi wa watumwa waliotupwa India “Jamii ya Siddis wenye asilia na damu za Afrika Mashariki waliachwa katika msitu wa jimbo la Karnataka nchini India baada ya biashara ya utumwa kukomeshwa mnamo 1848.
Wahindi hawajawakubali na sasa watamani kurudi kwao lakini wataenda wapi?” vizazi hawa Siddis wa watumwa kutoka aidha Kenya au Tanzania wapo zaidi ya elfu hamsini (50,000).
Zaidi yao 16,000 wanapatikana katika eneo la Karnataka, kundi lingine likiwa sehemu ya Gujarat huku wengine 12,000 wakiwa katika wilaya ya Junagadh.
Kundi la Siddis wapatao 10,000 wanapigwa ukope maeneo ya Hyderabad, Telangana pamoja na wale wanapotakina miji ya Goa na Maharashtra.
Hali kadhalika kunao Siddis ambao wamesonga mbele kwa ndoto zao za kimaisha hususani wale wanaotaka kujiendeleza katika michezo ya soka na kadhalika na kuwepo zaidi yao 25,000 nchini Pakistan maeneo ya Baloch ama Sindhi.
Wengi wa wanamichezo hatahivyo wamepiga kambi miji ya Lyari kuelekea mji wa Karachi. Kwa kuwa pia wengi wao wamekuwa na mazoea ya kuishi karibu na ufuo wa bahari kwa shughuli zao za kiuchumi, wengine wa Siddis wako nchini Sri Lanka katika miji ya Negambo, Trincomalee na Batticaloa.
Licha ya vilio vya Waafrika hawa kutoka Afrika Mashariki kwamba wangetaka kujumuisha pamoja na vizazi vyao ili kujua mizizi kama ilivyo kwa Wahindi waliopo Kenya na Uingereza na India, Umoja wa Bara la Afrika, (AU) bado halijathubutu kufungua mwanya suala hili.