Ni dhiki kwa bishara ya nyama ya ‘Punda’ nchini

Loading Article...

For the best experience, please enable JavaScript in your browser settings.

Maisha yake Pauline Kiryali yalisimama wakati punda wake wawili waliibiwa kutoka Kakululo, Kaunti ya Kitui, na kwa kuwa yeye ni mama mzee na mwenye ulemavu, changamoto za kulea watoto watatu kupitia pesa iliyopatikana kutokana na biashara hiyo ndogo ya punda zikawa maradufu; ku? kia sasa, yeye hutegemea pakubwa msaada kutoka kwa majirani. “Niliamka asubuhi moja kukuta punda wangu hawapo, niliamua kuwatafuta, nilifuata nyayo zao ambazo zilinielekeza kwenye kona yakushoto zaidi ya shamba langu ambapo nilipata minofu ya punda hao, ngozi yao ilikuwa tayari ishatolewa,” alisimulia PAMBAZUKO.

“Nikachanganyikiwa bila kujua maisha yangu yangekuwaje bila punda hao ambao walikuwa nwananipatia riziki” anaongeza akisema kuwa punda ndio chanzo kikuu cha mapato yake. “Punda wangu walikuwa wakinisaidia kwa njia nyingi; kuyachota maji, kwa kilimo, kusa? risha mazao ya shamba kutoka shambani hadi sokoni; kazi yangu ilifanywa rahisi na punda wangu, “anaelezea akiomboleza kwamba maisha yake yamebadilika tangu wakati huo.

“Sasa ninaishi maisha magumu sana, ulemavu wangu hufanya hali kuwa hata mbaya zaidi, ikiwa naweza kupata mfadhili atakayeokoa hali yangu kwa kuninunulia punda mwingine, naweza kurejelea biashara yangu ya kuchota maji kwa wakaazi hapa, vilevile naweza kumkodisha punda kwa wahudumu na kupata mapato zaidi,” anaongeza Kiryali.  

Kiryali hayuko peke yake, Stephen Ngugi, mfanyikazi mashuhuri wa punda kutoka Zambezi, Kiambu ni mtegemewa kwa kuwatafutia riziki wanawe watatu pamoja na bibiye, yeye pia ni mwathirika wa wizi wa kile anachukulia hazina yake kubwa.

 “Asubuhi ya tarehe 24 Januari 2018 inabakia kwenye ? kira zangu; nilipokuwa najiandaa kufanya usa? rishaji wangu wa kila siku, nilienda kuchukua punda wangu kwenye chumba chao ambapo nilipata mlango wa makao hayo ulikuwa umevunjwa na punda wangu sita walikuwa wameibiwa, tulijawa na huzuni kwani punda hao ndio chanzo chetu cha mapato,” anasema.

 Aliongeza kwamba ililazimika kutumia akiba aliyokuwa amewekeza ili kupanua nyumba yake kwa kuwanunua punda watatu ili kuirejelea biashara yake.

 “Nilitumia pesa zote kununua punda watatu ili kuendelea na biashara yangu, cha kusikitisha, miezi mitano baadaye, nilipokuwa nimeanza kupata utulivu, bahati mbaya nyingine iligonga na nikapoteza punda wote watatu,” anakumbuka kwa hasira.

 “Ikizingatiwa kuwa maisha yangu yote sijawahi kuajiriwa, familia yangu hutegemea mafanikio yatokanayo na biashara yangu hii, mimi huwawezesha watoto wangu kwenda shule nzuri, kuwalisha pamoja na kujenga nyumba tnayoiishi,” anaongeza.

Ngugi hivi sasa anafanya kazi ya mjengo katika eneo la ujenzi kama mfanyakazi wa kawaida, jambo analosema halijaweza kutimiza majukumu yake ya kifedha ya familia. Mwathiriwa mwingine Paul Ng’anga kutoka Nakuru kwa sasa ameajiriwa kama mwendeshaji pikipiki baada ya kupoteza punda wake wawili.

 “Wakati nilimpoteza punda wangu, niliambulia patupu maishani. Nilianza kuhangaika kuhusu nitakakopata pesa za kulipa kodi ya nyumba, kununua chakula na ada ya shule kwa watoto wangu watatu,” anasema.

Patrick Wansoni kiongozi wa vijana kutoka Mwea, Kaunti ya Kirinyaga anasimulia utovu wa ajira kati ya vijana huko Mwea kufuatia wizi wa punda ambao anachukulia kama ‘mwajiri sawa.’ “Kikundi chetu cha ustawi wa punda kimeathiriwa sana na ongezeko la wizi wa punda; tulikuwa tukimiliki takriban punda 125 lakini tangu nyumba za kuchinjia kufunguliwa, idadi hiyo imeshuka hadi 29,” aliliambia gazeti la PAMBAZUKO.

Anasema zaidi kwamba kuongezeka kwa mahitaji ya punda na bidhaa zake kumepelekea kuwepo na bei ghali ya wanyama hao hivyo basi kuifanya vigumu kwa wamiliki kuwarejesha punda waliopotea.

“Wengi wetu sasa wamebakia kuwa masikini na kuathirika kwa kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kinachosababisha baadhi yetu kuamua kutumia dawa za kulevya na pombe ili kukabiliana na hali ya kukata tamaa,” alisema.

Wahasiriwa wengine ni pamoja na Josephine Njuguna kutoka Nyandarua, Joseph Njogu kutoka Nakuru, Edwin Gitau kutoka Naivasha na Nalan’gu Nkuyayu kutoka Kaunti ya Narok ambao wote wanakadiria hasara iliyosababishwa na wizi wa punda wao. Wafanyabiashara wengi kutoka sehemu kame na zenye ukame wa nchi walijiunga na mamia ya wamiliki wengine wa punda kutoka Afrika na Asia kujadilia suala la maslahi na ustawi wa punda.

Waliungana jijini Nairobi wakati wa Kongamano la Biashara ya Ngozi za Punda almaarufu ‘Donkey Skin Trade Conference,’ 2019 ambalo lilifanyika chini ya idhini ya Mamlaka ya Kisekta za Serikali juu ya Maendeleo, IGAD kwa ushirikiano na Brooke East Africa.

Wakulima hao, ambao hutegemea wanyama hao kupata riziki kwa kufanya shughuli mbali mbali za kiuchumi kote nchini walitaka serikali kupiga marufuku biashara ya punda na  ngozi ya punda na kufungwa mara moja kwa vichinjio vya punda ili kuzuia kutoweka kwa punda kunakosababisha uzorotaji wa uchumi.

 “Mkutano huu umewaleta pamoja wajumbe wanaoshughulikia maslahi ya punda ili kuanzisha mazungumzo na uhamasishaji juu ya athari fupi na ya muda mrefu ya biashara ya ngozi ya punda,” alibainisha Eric Kimani, Mwenyekiti wa Bodi, Brooke Afrika Mashariki ambayo hutetea punda.   Miongoni mwa mapendekezo ya kongamano hilo ilikuwa ni pamoja na uundaji wa sheria za kudhibiti kuchinja punda hadi mpango wa kuwazalisha na kuwazidisha utakapowekwa pamoja na kuwa na ukaguzi wa idadi ya punda ili kutilia mkazo sheria na kanuni zilizowekwa.

 “Maazimio ya ujumbe huu yanatoa nafasi ya kuzungumzia kupiga marufuku biashara ya punda na ngozi  za punda kupitia sera sahihi na uundaji wa sheria dhabiti,” aliongeza Kimani. Wajumbe hao walitaka uhamasishaji zaidi kwa jamii juu ya athari za kuchinjwa kwa punda kwenye jamii, uchumi pamoja na hitaji la lishe sahihi na utunzaji mzuri kwa wanyama hao.

 Kulingana na takwimu kutoka Jumuiya ya Mifugo na Kilimo Kenya (KALRO), punda 301, 197 walichinjwa tangu kuamuru nyumba za kuwauza nje; asilimia 6.9 waliuawa mnamo 2016, asilimia 40.3 mnamo 2017 na asilimia 52.8 mnamo 2018. Uchanganuzi zaidi wa data zaidi unaonyesha utofauti wa punda 21, 030 kati ya vituo vya utekaji nyara na rekodi ya takwimu za kitaifa ya nchini (KNBS.)