Je, Magufuli ni mgema alotia pombe maji

Loading Article...

For the best experience, please enable JavaScript in your browser settings.

Rais John Pombe Magufuli.

Ngoma ikilia sana hupasuka na tamu ikizidi sana huchachuka na hata kuwa chungu kama shubiri. Hapa twamzunguzia rais jirani wa Tanzania John Pombe Magufuli ama kama Wabongo wanavyomita ‘Uncle Magu’ ama ‘JPM’. Bwana huyu alikuja kwa vishindo vikuu vya kuleta mabadiliko makuu Tanzania.Aliwashtua wengi kwa kupigana kwa jino na kucha dhidi ya zimwi la u?sadi. Tofauti na mtangulizi wake Jakaya Mrisho Kikwete alopenda anasa za kutembea kama mtalii  duniani ‘uncle Magu ‘ hana upuuzi huo kwani hakupenda starehe za kitalii za kupanda ndege.

Tukimgusia Kikwete ni kuwa alikuwa kiongozi aliyependa sifa na kujirembesha kwa masuti makubwa makubwa Kikwete alikuwa kama msanii alijirembesha kitanashati na kunyowa kama kijana wa kizazi kipya huku akitabasamu ovyo ovyo kama bwana harusi. Bwana msa?  huyu alikuwa daima na masafari yasoisha ya kile alichoita safari za kuleta maendeleo na mfano wa Tanania.

Kikwete hata alitembelea uga wa timu za Real Madrid na Barcelona wa Camp Noun a Santiago Bernabeau na kuwasi? a watanzani alipotoka huko eti ni uga mzuri huku u? sadi ukikithiri nyumbani! Magufuli alipochukuwa utawala aliondowa sikukuu ya uhuru na badala yake kuamrisha viongozi kuongoza mchakacho katika usa?  wa mazingira siku hiyo. ‘Haina haja kusherehekea tukitumia mamilioni huku mazingira ni machafu’ alingurumma Magufuli akiongoza usa?  Dar-es-Salaam.

Katika falsafa yake ya kauli mbiyu ya ‘hapa kazi tu’ bwana huyu mfupi wa miwani kama daktari wa kijerumani amewafuta  maa? sa wa serikali wa? sadi waliozembea kazini. Alikuwa kila mara akizuru ghafla katika a? si za serikali na kukaguwa ufanyikazi.Alimfuta a? sa yoyote aliyempata na kosa. Hata hivyo, kosa kubwa la Magufuli ni kuwapiga vita waandishi wa habari. Alimtia ndani muandishi mashuhuri Erick Kabendera ambaye aliandika habari za kumkosoa.

Jumuiya ya ulimwengu imeshutumu Magufuli kwa kumfunga Kabendera na kumuwekea mashtaka ya uwongo kama uraia, uhaini na u? sadi ili kumnyamazisha kwa kumpa kwelichungu. Waandishi wa habari wameteseka sana tangu Magufuli aingie madarakani mwaka 2015 kwani amepiga maarufuku magazeti yanayokosoa serikali. Magufuli alipiga marufuku magazeti ya ‘Mwanahalisi’ na ‘Mawio’ kwa kukosoa sera mbovu za serikali na udikteta dhidi ya wapinzani. Baadhi ya wandishi waliodhulumiwa na Magufuli ni Simon Mhina na jabir Idrissa. Tume ya Afrika ya wahariri tayari wamemuandikia Magufuli barua amuache huru Kabendera anayehishimiwa duniani.

Dhulma dhidi ya waandishi habari imeharibu sifa ya Tanzania inayoonekana kupinga uhuru na haki za maoni. Aghalabu serikali ya Tanzania hu? cha habari zote mbaya na kutaka mazuri tu.Majuzi Tanzania ililaumiwa ku? cha kisa cha wagonjwa walopatikana na athari za gonjwa baya la Ebola kule Dar. Kimsingi, Magufuli alosi? wa sasa amekuwa nduma kuwili na kugandamiza waandishi ambao wengi wamepotea na kufungwa.Aidha amekuwa dikteta kiongozi wa kiimla. Amegeuka yule mgema alosi? wa kutayarisha pombe nzuri kwa kuweka maji. Kinaya ni kuwa jina lake la kati bwana huyu ni hiyo hiyo pombe ya sifa!