Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa na mshikaji wake Geofrey Okuto Otieno walivamia boma la mwakilishi wa wadi ya Ganda, Reuben Katana siku moja kabla ya uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 17, Oktoba.
Jumwa alikiuka mila na desturi za kijamii kwa kujitosa mkutano wa wenyewe kwenye boma la watu na kuanza kuwacharaza wanaume mako? yaliyosindikizwa na cheche za matusi.
Vurumai kama inavyoshuhudiwa katika picha za video, zadhihirisha vurumai ambalo mwishowe, lilisababisha mauti ya mwanachama sugu na mwaminifu wa chama cha ODM, mwendazake Ngumbao Jola.
Jola aliuawa kufuatia vurumai iliyosababishwa na mbunge wake wa Malindi mbele ya maa? sa wa polisi na viongozi wengine.
Masaa kadhaa baadaye, Aisha Jumwa na Geofrey Okuto walikamatwa wakiwa nyumbani mwa mbunge Kakuyuni wakitafakari yaliyojiri.
Nani muaji wa Jola?
Licha ya uchunguzi kuwa unaendelea na idara husika, wengi hususan jamii ya Ganda inasononeshwa na hatua ya mahakama ya kuwaachilia wahusika wakuu, Aisha Jumwa na Geofrey Okuto ambao wadadisi wanasema kwamba kuwepo nje kunao uwezekano wa kulegeza jitihada za kuupata ukweli juu ya mauaji ya Jola.
Huku Wakenya wakitafakari yanayomngoja Aisha Jumwa na mshikaji wake baada ya kesi, habari zaidi zinajitokeza kumhusu kipenda roho chake kipya Geofrey Okuto kwamba ni mtu katili ambaye amewahi kuhusika na visanga vingi kuhusiana na vurumai za bunduki.
Duru zinaonyesha kwamba mnamo kwenye harakati za kampeini ya kura za 2017, kalameni huyu Okuto alikamatwa na polisi baada ya kuwafyatulia risasi wafuasi wa mpinzani wake mjini Nairobi.
Okuto Otieno na Aisha Jumwa walikutana kwa mara ya kwanza katika sherehe za chama cha ODM kusherehekea miaka kumi mjini Kisumu mnamo mwaka 2016.
Jamaa huyu kamwe si mgeni na vituko vya bunduki. Wengi waliomdhania kuwa pengine ni afisa wa polisi, walishangaa hatimaye walipopata rekodi rasmi za idara husika kuwa siyo chochote ila raia wa cha wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017 kilichishuhudiwa kwenye kura za mchujo wa ODM eneo la Mathare. “Previously described by police in Nairobi as a “dangerous” man” (Polisi mjini Nairobi wamemuorodhesha kuwa miongoni mwa mtu hatari), imewahi kuandikwa na kawaida. Katika patashika lililosababisha mauaji ya Ganda, alikuwa miongoni mwa wahusika wakuu walioshikana bega kwa bege Aisha Jumwa.
Katika a? si za idara ya usalama mjini Nairobi, Idara ya polisi imekuwa imemworodhesha kama jamaa sugu na hatari kufuatia kisa chake vyombo vya habari.
Mashtaka yake ya awali yanasema wakati huo alienda mtaa wa Mathare 4B mnamo Aprili 23, 2017 akiwa na bunduki aina ya bastola kuwazushia bughudha wagombeaji wenzake waliokuwa wanahutubia wafuasi mabwana Seff Kibira na Kennedy Ooko maeneo ya Kasovo na Mucedo. Sawa na tabia sawia iliyoonekana Ganda, Okuto Otieno aliwafungia njia wagombeaji wenzake hivyo kuzua rabsha hadi kufyatua risasi kwa umati wa watu kiholela.
Hakimu mkazi Francis Andayi hatimaye aliwachilia huru kwa dhamana ya shilingi 30,000 peke yake.
Agizo la mahakama wakati huo pia ilikuwa ni kunyang’anywa haki ya kumiliki bastola (silaha). Swali sasa ni je, nani alimruhusu kumregeshea kibali cha bunduki tena hadi kufikia kiwango cha kuwa mshukiwa mkuu katika mauaji ya Ngumbao Jola? Mauaji ya Ganda Kulingana na Ushahidi wa upande wa mashtaka, polisi inasema inao ushahidi unaoonyesha kuwa Okuto Otieon alikuwa pamoja na Aisha na wengine anapodaiwa alifyatua risasi ovyo na wakati huo huo umati wa watu wakaanza kulia kwamba Ngumbao Jola amepigwa risasi.
Stay informed. Subscribe to our newsletter
Baada ya Aisha na Okuto kukamatwa nyumbani Kakuyuni, walizawadiwa kupelekewa kunguni tu kwa siku mbili katika korokoro za bandarini kabla ya kuachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi laki tano (Sh500, 000) na kutejea makwao kula minofu ilhali Watoto wa Ngumbao Jola na jamii wakiwewesekea majonzi.
Mashtaka yake ya awali yanasema wakati huo alienda mtaa wa Mathare 4B mnamo Aprili 23, 2017 akiwa na bunduki aina ya bastola kuwazushia bughudha wagombeaji wenzake waliokuwa wanahutubia wafuasi mabwana Seff Kibira na Kennedy Ooko maeneo ya Kasovo na Mucedo.
Mshikaji mpya Geofrey Okuto Otieno kulingana na wafuasi wa karibu wa ODM, wanasema huenda akawa ndiyo ngome mpya ya upendo katika roho ya mbunge wa Malindi. Uhusiano wao ulianza wakati walipokutana kwa mara ya kwanza akiwa ni mwakilishi wa kina mama wa kaunti ya Kilifi, walipofyatuliana macho kule Kisumu walipokuwa wakisherehekea miaka 10 ya ODM. Kabla ya Gavana Evans Kidero kubanduliwa kaunti ya Nairobi, Okuto alikuwa miongoni mwa wasaidizi wa karibu na miongoni mwa mashahidi 13 katika kumpongeza Kidero ushindi wake wa 2013.
Wale mabwana ambao wanalalamika wameachwa na Aisha Jumwa, wanamtaja Okuto kama mtu aliyembana sana Aisha na wao kuporomoshwa inje.
Katika vitongoji vingi vya kwao Karachuonyo kaunti ya Homa Bay, watani wake wanamtambua kama “Mista Jeff” ilhali katika maeno ya Kilifi kwa wale ambao kwanza hawakumtambua mapema, walidhani mheshimiwa wao wa Malindi, amempata mume kutoka Nigeria (Naija) kutokana na mavazi yake aliyojitambulisha nayo daima dawama.
Tangu kura zilizopita za 2017, Okuto ndiye ambaye amekuwa akiandamana naye kwenye hafla zote za kisiasa nchini.
Wengine walimdhania ni dereva, mlinzi, msaidizi lakini ukweli sasa umejitokeza kuwa ni zaidi yah apo kwani kipenda roho hula hata nyama mbichi.