Alifahamika kama mkuu wa wafanyikazi wa umma na katibu wa kudumu katika A?si ya Rais na katibu wa baraza la mawaziri aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika serikali ya rais mwanzilishi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta.
Geoffrey Kariithi Karekia, maarufu G.K. alichukua hatamu za uongozi kutoka kwa mwenzake Duncan Ndegwa mnamo 1967.
Kando na kushikilia usukani kwenye huduma ya umma iliyogubikwa na mazingira yenye machafuko ya nyakati hizo yakiwemo unyakuzi wa mashamba bora ya maeneo ya milimani, almaarufu White Highlands, kuzuka kwa uhasama wa kisiasa, vita vya kuhamahama, machafuko kufuatia jaribio la kuigeuza serikali na kumngatua rais uongozini mnamo 197.
Kudhoo? ka kwa afya ya Rais Kenyatta, pamoja na kifo chake mnamo mwaka wa 1978, ni dhairi kwamba Kariithi alikuwa sio tu mwandani wa karibu wa Kenyatta ila pia alihudumu kama mshauri wa kutegemewa kuliko makatibu wengine wa wakati wake.
Itakumbukwa kuwa ni wakati Kariithi akiwa madarakani mnamo 1975 ambapo mauaji ya mwanasiasa maarufu JM Kariuki yalishuhudiwa pamoja na kushika kasi kwa kampeni ya mabadiliko ya katiba kabla ya kifo cha Kenyatta.
Rais wa zamani Kibaki alimuomboleza marehemu Kariithi kama “Mkenya mwenye nguvu na painia wa wafanyikazi wa serikali nchini na kiongozi aliyekorea Zaidi kama mhudumu wa umma.”
“Kariithi alisimamia huduma ya umma kwa ufanisi katika nyakati zenye msukosuko katika historia yetu ya kitaifa.
Kwa wakati huu wote, Kariithi alidumisha viwango vya hali ya juu katika kazi yake na alionyesha sifa bora kama mtumishi wa umma mwaminifu na aliyejitolea,”
Kibaki alitamka katika mazishi ya mwendazake. Aidha, Kibaki alimmiminia sifa kochokocho Kariithi kama aliyekuwa nadhifu na mwenye utaratibu kazini.
“Mzee Jomo Kenyatta alikuwa akitambua kwamba akiwa na Kariithi ana mtu anayeaminika na ambaye angemtegemea kwa ushauri na maamuzi ya busara,” akaongeza Kibaki.
Haya yanadhihirishwa na matukio kadha katika historia ya nchi na ambayo baadhi yalimhusisha Karithi kwa kina.
Kwa mfano, Kariithi alikuwa amemshauri rais Kenyatta dhidi ya kusa?ri kwenda Kisumu kufungua Hospitali mpya ya Russia mnamo siku ya Jumamosi Oktoba 25, mwaka 1969 sambamba na viashiria vya ujasusi na usalama kwamba ziara hiyo ingekumbwa na upinzani.
Kenyatta alimpuuza akisema Kisumu ilikuwa nchini Kenya na kuwa yeye alikuwa ni Rais wa Kenya na kuwa hangeogopa ku? ka pale abadan katan. Kilichoshuhudiwa baada yake kuwasili ni kizaazaa kilichowapelekea takriban watu 50 kuyapoteza maisha yao huku mamia wakiponea na majeraha kwenye vuta nikuvute iliyosababishwa na hisia tofauti kati ya rais Kenyatta na aliyekuwa naibu wake Jaramogi Oginga Odinga.
Ni msukosuko uliowazimu maa? sa wa polisi wa kitengo cha kumlinda rais, kwa amri ya Kenyatta, kuutawanya umati uliokuwa mahala pale kwa kufyatua risasi kiholela na kuwaangamiza wananchi.
Ziara ya rais Kenyatta ya siku pili kwenye Magharibi mwa Kenya, ilishuhudiwa miaka mitatu baada ya Jaramogi Oginga kushinikiza kukihama chama tawala cha Kanu, na kuunda Umoja wa Watu wa Kenya (KPU) mnamo 1966.
Stay informed. Subscribe to our newsletter
Na kwa kuwa Bw Odinga alikuwa na umaarufu mkubwa katika gome hilo, ilitazamiwa kuwa ha? a hiyo ya Kenyatta ingekumbwa na utata na mtafaruku wa aina yake.
Hisia za mauaji haya zimezidi kusisimua chuki na ugomvi wa kikabila kati ya kabila la Kenyatta la Kikuyu na lile la Odinga la Luo.
Hata hivyo, hilo huenda likasuluhishwa na hatua ya kushikana kwa mikono hivi karibuni kati ya Rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani na Kiongozi wa Cord Raila Odinga, ambayo inakusudia kuwaunganisha Wakenya wote na kumaliza ukabila.
Miaka ya mapema ya Kariithi Kariithi alizaliwa na marehemu Karunguru wa Mugo (Karekia) na Njoki Karekia, katika eneo la Njuku Wilaya ya Gichugu katika Kaunti ya Kirinyaga Mei mnamo mwaka wa 1925. Alikuwa na kaka na dada kadhaa ambao ni; Karungari, Wambere (ambaye alifariki na umri wa zaidi ya miaka 100), Nderu, Wakabu, Wacuka na Ngari (kaka yake mdogo) wote marehemu.
GK alijiunga na shule rasmi mnamo 1937 akiwa na umri wa miaka 12 Kabla ya hapo, alikuwa akihusika katika kutunza kondoo na mbuzi za baba yake.
Mwalimu wake wa kwanza Samweli Kaburo (anayejulikana pia kama Kathenge) alikuwa mmoja wa waongofu wachache Wakristo-Wakiafrika katika utoto wa GK.
Darasa lao lilijengwa na Magoto (nyuzi kavu za ndizi) na Magoko (gome la miti ya kitamaduni). Mwalimu mwingine aliyechangia pakubwa katika kulainisha maisha ya GK alikuwa Mwalimu Gladstone ambaye pia alikua mshauri wake wakati wa ujana wake.
Baada ya kugura Mugumo mnamo 1939 alihudhuria shule za Gatugura na Gatunguru kabla ya kujiunga na Shule ya Kagumo kwa elimu ya ziada hadi mwaka wa 1942.
Kagumo ilikuwa taasisi ya kifahari ambapo nafasi chache zilizopatikana zilikuwisha kutengewa wanafunzi tu wenye ueledi wa hali ya juu.
Mnamo mwaka wa 1944, Kariithi aliweza kumzika babaye mzazi kwenye tukio lililoelezewa kama nadra kwani siku hizo, wafu walikuwa wakitupwa kwenye vichaka na kuachiwa ?si wawale.
Kujiunga na Alliance Kutoka Kagumo, Kariithi alijiunga na shule ya upili aliyoitamani ya Alliance mwaka wa 1945 ambapo mtajika wa somo la hesabu, Carey Francis, alikuwa mwalimu mkuu. Nambari yake ya usajili ilikuwa ni 835.
Kufuatia hali yake ya uchochole, Kariithi alipata ufadhili wa karo kupitia burari iliyotoka kwa Halmashauri ya Afrika ya Wilaya ya Embu (EADC) Miongoni mwa wengine waliojumuika naye ni pamoja na Walter Njiru, Johnson Gituma, Duncan Ndegwa, Kariuki Gechau, Profesa Bethwel Ogot, Profesa Wasawo, marehemu Dkt.
Gikonyo Kiano, marehemu Dkt. Taita Towett, na marehemu Robert Matano.
Alliance ilifungua macho ya Kariithi kwa utofauti wa nchi yake na ni uzoefu huu ulikuwa wenye msaada wakati wa kazi yake katika Huduma ya umma, uraia, na baadaye maishani mwake.
Ni pale ambapo usikivu wa kisiasa wa GK, uongozi na ujuzi wa watu ulitunzwa.
Alikuwa mwanachama na mwenyekiti wa kongamano la wanafunzi na baadaye akateuliwa kama mkuu wa vinara na nahodha wa Chumba cha Livingstone.