Tishio Kubwa kwa Naibu Rais William Samoei Ruto na “Team Tangatanga” sio kiongozi wa upinzani Raila Odinga bali ni Fred Matiang’i. Waziri huyo kiranja na Usalama wa Ndani ana wakosesha raha wanaRuto na nahodha wao wakihisi Matiang’i ni ? mbo ya UhuRaila 2022 kumzima mpendwa Kigogo chao Cha Mkoa wa Bonde la Ufa penyenye za kuwa Rais wa tano jamhuri hii chini ya makubaliano-siri 2013 baina URP ya Ruto na TNA ya Uhuru hatimaye kuundwa Jubilee Alliance ya sasa.
Bila shaka suluhu ya siri kati ya Uhuru na Raila mnamo Mei 9 mwaka Jana kufuatia vurugumechi za Uchaguzi mkuu 2017 umemweka Ruto na kigaro chake mataani. Kuja kwa Raila na waitifaki serikalini kumejenga ODM ya Baba Tinga na kummbomowa Ruto na wana-URP wa zamani na wengineo chini ya bendera ya Ruto nchini.
Raila na wenyeji-wageni wengineo angavu wa Rais wamejikuta chini ya mawimbi ya shutuma, matusi na kejeli za Team Tangatanga, lakini lakuudhi kwa wana-Ruto zaidi ni kuhisi Uhuru na Raila wakishambulia “waasi” hao wa Jubilee kwa mbinu za siri na dhahiri. Mmoja wa majamadari wa UhuRaila ni Waziri kiranja Fred Matiang’i.
Huyu bwana hapigani dhidi ya Team Tangatanga kiwaziwazi ama kisiri. Kinachomchongea mbele ya akina Ruto ni sifa na mafanikio yake yakumjenga Rais Uhuru na washirika-sugu wake (akiwemo Raila, hasimu mkubwa wa Naibu Rais) kupitia kusukuma mno Ajenda Kuu 4 za Rais na utendakazi Bora Wizara zote. Jambo linalomng’arisha mno Uhuru na mhandisheki mwenzake Raila ndani na nje ya Kenya.
Sifa kwa Matiang’i ni sifa kwa bosi wake Uhuru kama Rais aliekubuhu kimaendeleo, kimamlaka na kisiasa za wiano, suluhu na Handisheki. Matiang’i na mwana wa Rais mstaafu seneta Gideon Moi wa Baringo ni bakora-mbinu za Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga dhidi ya mahasidi wa “Handisheki” na UhuRaila 2022.
Ni wanamaji wawili watazamiwao kumkatia umeme Naibu Rais tuelekeapo 2022: Wana tajriba, weledi na ujasiri kuwatekelezea Uhuru na Raila kazi hiyo na zenginezo. Tofauti ni kuwa Matiang’i yumo serikalini huko Gideon akiwa nje kwa vile ni seneta na mwenyekiti wa KANU nchini. Matiang’i anasimamia utekelezaji na usimamizi wa miradi ya kitaifa chini ya Ruwaza 2030 wakati Gideon akipiga siasa kujijenga kama Rais mtarajiwa siku za usoni mbali na kusimamia mali, masilahi na taratibu zote za nani aruhusiwe ama asiruhusiwe kumuona Mzee Daniel Arap Moi nyumbani kwake.
Mbali na kusimamia mali, biashara na shughuli zake binafsi za kifamilia pamoja na zile za KANU nchini, Gideon Moi pia kampeni ya kujumuika na wafuasi, wakaazi wa eneo la Baringo analowawakilisha kama seneta pamoja na viongozi, maa? sa na wakuu wengineo wa mashirika, serikali na jumuiya ya wanadiplomasia.
Hii inamfanya ?mbo ya mbali kwa namna fulani tofauti na Matiang’i ambaye angavu zake ni za Waziri asiye mwanasiasa wakuchaguliwa kikura kama ilivyo kwa mawaziri wenzake serikalini. Ngangari nzima za Matiang’i zilionekana majuzi alipohudhuria sherehe rasmi ya kuunganisha vikosi vya maa? sa tawala na polisi wa kawaida Chuo Cha mafunzo Administration Police Training College Eastleigh jijini Nairobi. Akihutubia waandishi baada ya ha? a hiyo aliyachapa makampuni ya kamari za spoti kwa kutofuata sheria na taratibu za huduma mashinani akinguruma.
“Yeyote anaeshughulika (katika sekta hii) lazima akaonyeshe leseni rasmi kwa Mkuu wa polisi mkoani na kaunti anakoendesha biashara hiyo. Kinyume na hivyo, atakuwa anaendeleza uhalifu,” akawika Matiang’i.
Bodi ya kudhibiti na kuhalilisha shughuli za kamari nchini (Betting Control and Licensing Board) imedinda kuribiza leseni za kila mwaka kwa kipindi 2019/ 2020 kwa zaidi ya makampuni binafsi 27 hadi yatakapotimiza vipengee endelevu vya sheria ikiwemo kulipa jumla ya shillingi bilioni 11 kama ada ya kodi kwa Mamlaka Ya Ukusanyaji Ushuru nchini KRA .
Yasemekana SportPesa, Betin na makampuni wenza zinatumia bilioni 91 na nusu pesa za Kenya kujitangaza mitandao ya Safaricom katika sekta yenye thamani ya bilioni 200 pesa za Kenya. Wanaomjua Matiang’i alivyonyorosha vichwamaji kwenye sekta ya Elimu wana shaka kama “machakaramu” wa kamari na mahasimu wa Handisheki ya UhuRaila watatoboa dhidi ya Waziri huyu wa Usalama wa Ndani.
Matiang’i Kama Waziri wa Elimu nyakati hizo alizima u?sadi, utepetevu wa utendakazi, ukabila na udanganyifu sugu wa mitihani ya kitaifa na mfumo wa daraja za mashule kwenye mitihani hiyo. Ni sifa kochokocho anazoonekana kuzikamia kuzipata kwenye wadhfa wake wa sasa wa kudhibiti changamoto zozote zinazotishia Usalama na utangamano ndani ya mipaka ya Kenya kutokamana na matamshi na nyendo za walalahai na walalahai nchini. Tayari ametiana mieleka na Kamati za bunge la kitaifa na seneti kuhusu uzembe wa kuhoji na kuta?ti washukiwa wa u?sadi
Idara za serikali
Amevurugana na Mawaziri kadhaa na kuebuka kidedea Kama ambavyo anatarajiwa kusambambaratisha jamaa za Tangatanga wanaotaka ajiuzulu kwa madai ya u? sadi na “kashfa” ya kuwaondolea ulinzi wabunge na maseneta wanaoegemea upande wa Ruto. Si ajabu akina mbunge wa Kipsaret Oscar Sudi na seneta Markomen hawakomi kumpamba Matiang’i kama mshika? mbo wa Handicheki (hand cheque) na sio Handisheki (handshake) alietumwa na Uhuru na Raila.
Fundi hodari
Stay informed. Subscribe to our newsletter
Sudi na Markomen hawakukosea: Matiang’i si Sarangi tu wa serikali, ni fundi mangungu anaedimkadimka na kupiga ngoma za UhuRaila 2022 mbele na nyuma kulala na kuamka. Wengi wanaomfananisha na marehemu Simeon Nyachae wanaho? a ngangari zake serikalini huenda zikaishia ukingoni kama mkisii mwenzake huyo alivyofura ikulu ya Arap Moi Kama povu la sabuni kabla kutupwa mtaro wa maji-taka na hatimaye ku? lia nje ya serikali na kuzikwa kaburi la sahau kisiasa. Kwa sasa mgogo huyo amekuwa akisi? wa na kutetewa hadharani na Rais wa nchi pamoja na kiongozi wa upinzani ambaye ni Waziri mkuu wa zamani.
Haijalishi kuwa katibu mkuu wa Matiang’i huyuhuyu (Karanja Kibicho) kwa sasa amezongwa na wingu la tuhuma katika kile kinachosemekana na wana-Ruto kama njama za kummuwa Naibu Rais William Ruto. Je, haya ni yaleyale ya waswahili waliosema apigae kuku ataka mwenye-kuku? Yote hayo si hoja wala ajabu, Matiang’i hajakuwa wa mwanzo kuitia bahari chumvi -- hayo ni ya Mola moliwa muumba juu na chini na vilivyomo baina yao.