Leo tutazungumzia magonjwa ambayo yanaweza kuwa hatari kwa wajawazito. Pumu, ugonjwa wa kisukari na kuwa katika hali ya kudhikika moyoni, vyaweza kudhuru afya ya mwanamke na mtoto wakati wa uja uzito kama hali hizo hazitashughulikiwa vilivyo. Mimba inaweza kusababisha hesabu ya chembe chembe nyekundu za damu kupungua na kusababisha ugonjwa wa anemia ambao una maana ya damu kupungua na kupata machovu na mwili kubadilika rangi na kuwa mweupe.
Tatizo jingine hutokea wakati mbegu ya uzazi inapojibanza mahali nje ya mfuko wa uzazi, na kutatiza kukua kwa mtoto. Jambo la kufurahisha ni kwamba wataalamu wa matibabu wana ufahamu wa kukabiliana na matatizo hayo ya kiafya yanayozuka wakati wa uja uzito.
Magonjwa ya mfumo wa ulinzi
Magonjwa ya mfumo wa ulinzi hutokea wakati chembe chembe za mwili zinazokabiliana na vitisho dhidi ya afya kama vile virusi vinaposhambulia chembe chembe zenye afya.
Huku hali hiyo ikizidi kuendelea miongoni mwa wanadamu, wataalamu wa utafiti wamepigwa na bumbuazi wasijue ni kwa nini hali hiyo huwavamia wanawake zaidi. Huku kukiwa na aina nyingi za magonjwa yanayoshambulia mfumo wa ulinzi, dalili zinazowapata wengi ni pamoja na kuchoka, homa hafifu, ngozi kuwasha na kisunzi au kisulisuli.
Sehemu kubwa ya mfumo ulinzi ina makao yake tumboni. Wengi anaojipata katika hali hii ya maradhi wamegeukia tiba ya kawaida kama vile kupunguza kula sukari, kupunguza kula vyakula vya mafuta, kujiepusha na mawazo yenye kuleta dhiki, na kupunguza ulaji wa vitu vyenye chembe chembe za sumu. Hata hivyo kinga bora zaidi ya kukabiliana na magonjwa ya mfumo ulinzi ni kugundua mapema iwapo una maradhi hayo.
Ugonjwa unaosababisha mifupa kuwa dhaifu
Ugonjwa huu husababisha mifupa kuwa dhaifu na kuvunjika kwa urahisi.
Mambo kadhaa husababisha ugonjwa huu ambao huwakumba sana wanawake. Sababu hizo ni pamoja na umri, kulewa, baadhi ya dawa, chembe chembe za asili ya kimaumbile, ukosefu wa kufanya mazoezi, kuwa na mwili mdogo, kuvuta sigara na utumiaji wa vitu vinavyojulikana kama steroids yaani aina ya chembe chembe, Ili kupata kuugundua ugonjwa huu, wahudumu wa afya hupima uzito wa mifupa kwa kutumia mitambo ya X-ray na ya ultrasound.
Ingawa ugonjwa huu hauna dawa, wahudumu wa afya wanaweza kutoa matibabu ambayo yatazuia ugonjwa kuendelea. Hutumia nyongeza za kuimarisha za vipa nguvu vya kuimarisha ubora wa chakula, kuchagua mfumo wa kimaisha wenye kuimarisha afya, na pia kutoa madawa.
Dhiki za moyo na kutokuwa na utulivu
Chembe chembe za kawaida za kimaumbile zinapopanda na kushuka zinaweza kusababisha dhiki za moyo na kutokuwa na utulivu. Mkusanyiko mkubwa wa chembe chembe ambazo hutangulia siku za hedhi, hutokea sana kwa wanawake huku hitilafu zinazosababishwa na hedhi zikitoa dalili zinazofanana na hizo, lakini zinazokuja kwa wingi zaidi.
Muda mfupi tu baada ya kujufungua, wanawake wengi waliojifungua hupata aina fulani ya dhiki za moyo ambazo huwa na dalili kubwa zaidi, zenye kuzusha hali ya wasiwasi mkubwa. Hupatwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya mienendo huku kukiwa na hali ya wasiwasi, dhiki, kukasirika, kujihisi kuchoka na mengineyo.
Stay informed. Subscribe to our newsletter