Vigango 30 ambavyo viliibwa miongo kadhaa iliyopita na kupelekwa katika taifa la Marekani sasa vimeregeshwa humu nchini.
Kwa kawaida ya jamii ya wamijikenda, wakati wa sherehe kama hii, wahudhuria huangua kilio ambacho waombolezaji huamini wazi kuwa kinasaidia kuiweka mizimu ya mababu na mababu zao kufikiwa na kineme cha amani waliko lala pema peponi.
Vigango hivyo yadaiwa vilipotea katika hali tatanishi ambayo ilisababisha mahangaiko hasa kwa familia ambazo zilikuwa zimepoteza wapendwa wao.
Kwa kifupi, yaaminika viliibiwa na wazungu ambao licha ya kuvitumia kwa utafiti katika taasisi mbali mbali za turathi na utamaduni, yasemekana haikuwa rahisi kwao kwani daima viliwasumbua kwa jinamizi ndotoni wakisukumwa kimawazo waviregeshe kwao na mizimu ya waliokufa.
Akivikabi- dhi vigango hivyo kwa wazee wa Kimijikenda Waziri wa Michezo Utamaduni, Sanaa na Turathi za Kitaifa Balozi Amina Mohamed katika Makavazi ya Fort Jesus, amesema vigango hivyo ni ishara ya kuwa jamii za pwani zitaendela kuhifadhi tamaduni zake pamoja na jamii hiyo kuimarika zaidi.
“Vigango hivi ambayo vilikuwa vimepelekwa nchini Marekani miaka mingi iliyopita, na kuhifadhiwa huko Danver nchini Marekanai mwaka wa 2015 iliarifu taifa la Kenya kuwa inataka kuviregesha, hivyo basi kufikia tarehe 3 mwezi Julai mwaka huu vigango hivyo vikaregeshwa ,” akasema Waziri Amina.
Kulingana na waziri Amina vigango hivyo ambavyo vimeletwa humu nchini kwa gharana ya Danver Museum of Natural history ya nchini Marekani vimekuwa vikitumika kufanyiwa utafiti katika vyuo vikuu vya Amerika.
“Wakati vigango vilipotolewa humu nchi na kupelekwa Marekani, vigango hivyo vilikuwa vikitumiwa kama vitega uchumi na mapambo,” akaongeza Waziri Amina.
Inaamika baada ya kuibwa kwa vigango hivyo, jamii ya Mijikenda imekuwa ikishudia maafa ya kimaumbile ikiwa ni pamoja na ukame, na mifugo kufa katika hali ambayo haieleweki.
Waziri Amina hata hivyo ameyataka mataifa mengine ambayo bado yanahifadhi vigango visivyo kuwa vyao kuhakikisha kuwa wanawasiliana na wenyeji halali ili kuyakabidhi mataifa husika. Vigango vyengene 29 vilevile viko katika uwanja wa ndege jijini Nairobi vikusubiriwa kuletwa na kurudishwa kwa jamii husika ya Mijikenda.
Hata hivyo vigango hivyo vimekabidhiwa wazee wa mijikenda na vitapelekwa katika kaunti ya Kilifi ambako vigango hivyo yaaminika vilitoka miaka ya zamani.
Waziri wa tamaduni, Jamii na michezo katika kaunti ya Kilifi Mwenda Karisa amesema watakubalina na wezee wa Kaya wanaotambulikana kama “GOHU” ili kujua iwapo vitarejeshwa kwa wenyewe ama vitahifadhiwa mahali pamoja.
Mtu ambaye ni Gohu akiaga dunia wazee wa Gohu wanatengeneza kigango cha kumtambulisha kuwa alikuwa anamiliki wadhifa wa Gohu katika jamii ya giriama katika Kaya na kuwa mtu wa cheo kikubwa sana na .
“ Mimi nina hakika kabisa iwapo “Wakati vigango vilipotolewa humu nchi na kupelekwa Marekani, vigango hivyo vilikuwa vikitumiwa kama vitega uchumi na mapambo,” Waziri Amina Mohamed.
Vigango hivi vitapelekwa katika uwanja wa Karisa Maitha na jamii zilizopoteza vigango hivyo ziitwe na kufahamishwa kuwa vigango vyao vimeregeshwa ili wanaoweza kuvitambua wavitambue na kuvitwaa na kama hawatavitambua kufanywe mashauri ya hatua zitakazofuata baadaye,” akasema Mwanda.
Stay informed. Subscribe to our newsletter
Msemaji wa jamii ya wamjikenda Joseph Mwarandu ambaye pia ni wakili anasema kurudishwa kwa vigango hivyo kutaleta afueni kwa jamii hiyo na matatizo mengi huenda yatapungua.
“Hizi ni roho za watu wetu na ni wazee wa zamani na zimeleta shida hapa kwetu pamoja na huko Marekani ndio sababu vimerudhishwa,” akasema Mwarandu Jamii ya mijikenda inaamini kuwa kuna maisha baada ya kifo ambapo wazee wote walioaga dunia wanapaswa kuwa miongoni mwa watu ambao wanatambulika hadi kufikia sasa.
“Ndugu zetu wa mataifa ya walipoona vigango hivi vimenakshiwa kwa virembesho wakaona wavichukue na kuvihifadhi katika makavazi yao,” akaongeza Mwarandu.
Mwarandu anasema watu ambao walihusika kuvichukula walikuwa hawajua umuhimu wa vigango hivyo katika jamii hiyo, hali ambayo ilisababisha jamii husika kufanya tambiko ili masaibu yasikumbe jamii ya wamijikenda.
Hata hivyo inasemekana kuwa watu wote walihusika katika biashara hiyo ya kuuza vigango hivyo walikufa vifo kwa kimajabu na wengine kushikwa na wazimu pamoja na kupotea bila hata kupatikana. Kazungu wa Hawe Risa ambaye ni mshauri mkuu wa “WAGOHU” katika kanda ya pwani anasema kumekuwako na uhaba mkubwa sana wa Mgohu baada ya wazee wengi kuaga dunia.
Kazungu anawataka vijana wa kimijikenda kujitokeza ili kupokea mafunzo ili wakaweze kulinda tamaduni wa jamii ya wagiriama. “Wagohu ambao tumebaki tuko kidogo hivyo tunawataka vijana wetu wa kimijikenda kujitokeza ili kupata mafunzo ili waweze kulinda na kutunza tamaduni zetu ,” akasema Karisa.
Sio kila mti hutengenezwa vigongo hivyo kulingana na jamii ya wajikindea na miti hiyo hufifadhiwa na kutuzwa sana ili isiweze kupotea.