Huenda maeneo bunge zaidi ya 27 nchini yakavunjwa baada ya zoezi la sensa kukamilika mnamo mwezi Agosti.
Siyo habari njema kwa wengi lakini hali hii ndivyo ilivyo licha ya sheria za nchi zenye kugeuzwa kila uchao, hata maisha ya mwanaadamu yamo hatarini kwani so tulitoka kwa udongo na tutarudi wa huo udongo.
Hii ni kwa sababu ingawa katiba mpya imeeleza kwamba maeneo bunge ya taifa yatakuwa 290 tume huru ya uchaguzi na mipaka ya (IEBC) imepewa uhuru wa kugeuza mipaka na kupunguza maeneo bunge mengine na kuongeza kulingana na idadi ya watu itakayotokana na sensa.
Cha msingi kabisa kwenye mageuzi hayo ambayo yamkini yatakuwa na athari kubwa kisiasa na kimaendeleo ni kota ya idadi ya watu kwenye kila eneo bunge ambayo kutokana na sensa ya mnamo mwaka 2009 ni jumla ya watu 133,000.
Kota hii hutokana na kugawa idadi ya watu wote nchini na maeneo bunge 290. Maeneo bunge 27 Yote ni yazungumzwe lakini kunazo kaunti ambazo zitakuwa taabani iwapo hatua ya aina hiyo itatekeleza.
Pwani ni miongoni mwa maeneo ambayo kaunti za Lamu na Taita Taveta vile vile Tana River zinaweza kudhurika pakubwa. Wananchi wengine wa meaneo ya bunge ya Ndaragwa, Tetu, Mukurweini, Othaya, Kangema na Mathioya kutekea nyanda za Kenya ya kati hali kadhalika watapatwa na jembe la IEBC endapo sheria ya mipaka mipya itafuatwa baada ya sense za Agosti.
Wembe huo huo unasubiri kunyoa maeneo bunge ya Samburu East, Marakwet East, Keiyo North miongoni mwa mwengi ya ukanda wa Bonde la ufa. Magharib mwa Kenya, maeneo ya nyanda za kaskazini mashariki vile vile yameorodheshwa kutokana na udhaifu wake wa kuwa na idadi hitajika ya watu.
Hadi kufikia jana tukisubiri zoezi la sensa kufanyika na iwapo tume ya mipaka itatimiza haki yake hiyo basi ni maeneo yafuatayo yatakayoangamia; Voi, Mwatate, Wundanyi, Mwatate, Lamu East, Lamu West, Mvita, Bura, Galole, Ndaragwa, Tetu, Mukurweini, Othaya, Kangema, Mathioya, Samburu East, Marakwet East, Keiyo North, Mogotio, Vihiga, Budalangi, Isiolo South, Kilome, Laisamis, North Horr, Sakuna na Mbeere North.
Mfano ulivyo Huenda maeneo bunge yote 4 kwenye kaunti ya Taita Taveta yakavunjwa baada ya sensa ya kitaifa itakayoanza mwezi ujao. Kwa minajili hii hakuna eneo bunge hata moja kwenye kaunti ya Taita Taveta imefikisha idadi hii ya kota.
Voi ina idadi ya watu 87,803, Mwatate 73,168, Wundanyi 56,021 na Taveta 67,665. Ikieleweka kwamba kaunti ya Taita Taveta iko na watu wapatao 284,657, inamaanisha kwamba ni mae- “Zoezi la kuhesabu Wakenya la sen- sa huenda likatuletea habari za kuzikwa kwa maeneo 27 ya bunge nchini ikiwa ni pamoja na kudhuru kaunti za Nyeri, Taita, Kakamega, Baringo, Mombasa, Lamu miongoni mwa nyingine.” neo bunge 2 pekee yatakayobakia kama vile Taita na Taveta.
Hii itakuwa na athari kubwa kimaendeleo kwani mgao wa hazina ya CDF kwenye kaunti utapungua kwa nusu.
Eneo bunge la Mwatate ndilo changa zaidi kwani lilibuniwa kutoka eneo bunge la Wundanyi kabla ya uchaguzi wa 1988 huku mbunge wa kwanza akiwa Eliud Mcharo wa chama cha Kanu aliyekuwa mkuu wa elimu mkoani pwani hapo awali.
Mcharo alishinda kiti cha Mwatate mwaka 1992 bado akiwa kwa Kanu. Kwenye mwaka wa 1997 kiti hicho kilinyakuliwa na meja mstaafu Marsden Madoka wa Kanu. Madoka alishinda tena kiti hicho cha ubunge 2002 na kukiaga mwaka 2007 kiliponyakuliwa na Calist Mwatela aliyekuwa hapo awali mbunge wa jumuia ya Afrika Mashariki kule Arusha wa chama cha ODM.
Bw Mwatela ndiye mbunge wa pekee kukalia kiti hicho kwa muhula mmoja pekee kwani aliangushwa na Andrew Mwadime wa ODM mwaka wa 2013. Bwana Mwadime alishinda kiti hicho kwa mara ya pili mwaka wa 2017 hadi sasa.
Kama mageuzi ya mipaka baada ya sensa ya mwaka huu yatafaulu huenda wanasiasa wengine wakavipoteza viti hivyo na kustaafu siasa. Hata hivyo kuna dhana kwamba idadi ya watu isitumiwe peke yake kama kigezo cha kuvunja maeneo bunge huku wengi wakidai kwamba kuna maeneo bunge yenye watu wachache lakini eneo kubwa mraba hivyo kuwabidi wabunge kwenda mwendo mrefu wakiwahudumia wananchi.
Stay informed. Subscribe to our newsletter
Hata hivyo ni jambo la kukanganya inapodhihirika kwamba kuna maeneo bunge ambayo idadi ya watu inatoshana na kaunti nzima kwenye sehemu zingine nchini. Kwa mfano gavana wa gatuzi la Lamu lenye watu 101, 000 anapata mshahara na marupurupu sawa na gavana wa Kiambu yenye watu milioni 1.6.
Kwa misingi hiyo hiyo, mbunge wa Lamu mashariki yenye watu 20,000 anapata mshahara sawa na mbunge wa Eldoret kaskazini yenye watu zaidi ya 400,000 mara 20 zaidi ile ya Lamu mashariki. Kwa ujumla kuna maeneo bunge 27 ambayo huenda yakavunjiliwa mbali baada ya sensa ya mwaka huu zikiwemo.