Samboja kikapuni akielekea kwa Raila

JavaScript is disabled!

Please enable JavaScript to read this content.

Gavana wa Taita Taveta Granton Samboja na Kinara wa ODM Raila Odinga.

Wangwana wa kaunti ya Taita Taveta, nambari 006 kati ya kaunti 47 za Kenya wangali wamepigwa na butwaa wakati gavana wao Granton Samboja ambaye aliingia uongozini mwaka 2017 kwa tikiti ya kulazimishwa ya WIPER, alimkimbilia kiongozi wa upinzani Raila Odinga badala ya kinara wake wa chama Stephen Kalonzo Musyoka kwa ushauri wa dharura kuhusiana na kusambaratika kwa serikali yake kufuatia mjuvyo wa kiutawala baina yake na wawakilishi (MCAs) wa wadi za Taita Taveta.

Habari za kuaminika zatujia kinaga ubaga kwamba Gavana Samboja huenda akahamia rasmi kwa chama cha ODM siku chache zijazo kubwaga chama cha WIPER, tayari kwa vita vyovyote vile vya siasa ya uchaguzi mpya mdogo wa kaunti endapo pendekezo lake la kuitaka serikali ya kaunti ya Taita Taveta ivunjiliwe mbali litatimia.

Kuzuru kwake kwa kiongozi wa upinzani, alikuwa ni kupata hakikisho kuwa anaweza kusombezwa kwa tikiti ya ODM kwa uchaguzi mdogo ili amalize kipindi chake cha miaka michache iliyobakia alafu chama kitaamua nani atapendekezwa uchaguzi mkuu ujao wa 2022.

Sababu halisi ya kutaka kuhama WIPER bado haijajitokeza ila wachanganuzi wanasema kimya cha kiongozi wake Kalonzo Musyoka kuonyesha jitihada za kumkinga gavana wake zingali za kuweweseka tu.

Msimamo wa Raila Akizungumza muda mfupi baada ya kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na Samboja katika afi si zake maarufu za Capital Hill, kinara wa upinzani na kiongozi wa ODM, Raila Odinga ameonekana kumuunga mkono gavana huyo akisema kwamba lazima mazungumzo ya pande zote mbili zinazozozana za wabunge wa kaunti na gavana yafanyike ili kutoa loki inayozuia serikali hiyo ya kaunti kurejea hali yake ya kaiwaida.

Ingawa hivyo, Raila naye anaonekana kutowabembeleza wahusika hususan wabunge wa kaunti (MCAs) akisema kwamba iwapo wataendelea kuonyesha maringo, basi hakuna budi ila wapate funzo kwa serikali hiyo kuvunjiliwa mbali na kuitisha uchaguzi mpya wa viongozi wote.

“Ili liwe funzo hata kwa kaunti nyingine, nawarai wote wanaohusika kwenye mgogoro huu wa uongozi wa kaunti ya Taita Taveta kukaa kushauriana na kupata suluhu la kudumu kwa kipindi kilichobakia. Hatahivyo, wakizidi kuwa vishipa itibidi serikali ivunje watu wote warudi debeni,” anukuliwa Raila alipohutubia vyombo vya habari baada ya kukutana na Samboja.

Chanzo cha vurugu Chanzo cha gavana Granton Samboja na wabunge wake wa kaunti kuvurugana kulitokana na makadirio ya bajeti za wadi 20 za Taita Taveta ya shilingi 850 milioni mwaka huu wa 2019 ambapo gavana alidinda kuipitisha na kuiregesha kwa ukarabati zaidi.

Wabunge wa wadi zote 20 walikuwa na lazima ya kupitishiwa bajeti yao ya shilingi 41.5 milioni huku wengine 13 wateuliwa wakitaka kutengezwa kitita cha shilingi laki tano (500,000) kila mtu.

Dhambi la Samboja kwa wabunge wake wa kaunti, ni kutaka mapendekezo yao hayo kwanza yapitishwe na kamati maalum ya seneti ya fedha (Senate Public Accounts and Investment Committee) ili aweze kukubaliana nayo kisheria lau sivyo itabakia haramu kimsingi wa uwezo wa kaunti ulivyo sasa.

Hali hii yasemekana kumkera Raila Odinga ambaye analalamika kuwa hivyo ndivyo ugatuzi unavyoshikwa shingo na baadhi ya kaunti nchini.

“Yasikitisha kwamba ugatuzi ama ugavi wa raslimali unachomwa miba na kukosa kuafi kia malengo yake yaliyokusudiwa kikatiba kwa sababu ya malumbano nyanjani. Nimeelezea wasi wasi wangu huu kwa kaunti nyingine zilikokuwa na tatizo aina hii kama vile Nairobi, Kisumu, Mandera, Siaya na Mombasa,” asikitika kinara wa upinzani Odinga.

Anaongeza kusema kwamba anashangazwa na wabunge wa kaunti nchini ambao wamesahau majukumu yao ya kuwa wapekuzi na macho ya kulinda ugatuzi na badala yao kuingilia kazi ambazo haziwahusu kama za kupangia bajeti kaunti badala ya kuzipiga msasa kama wanavyotakiwa kufanya.

Kila kukicha anagutishwa kusikia kuwa wabunge wa kaunti wanawaendea kichichini magavana wao kuwavunja mikono ili wawapatie fedha ambazo hazimo kwenye makadirio ya matumizi yam waka.

Ndoa ya lazima Wale wadadisi wa siasa ya ndani katika kaunti yake, wanajijazia kwamba hata wakati alipokuwa ameshauriwa kuwania ugavana, kamwe Granton Samboja hakuwa amejipanga kiuongozi kwani licha ya msukumo wa kisiasa kutoka kwa wafuasi wake waliotaka mabadiliko ya uongozi wa kaunti, yaaminika daima alionyesha ishara kwamba viatu vya John Mruttu ama ugavana, ni vipana na kwake ni kubahatisha tu.

Awali, kabla ya aliyekuwa seneta wa Taita Taveta (2013-2017) Danson Mwazo alipokuwa akitongozwa na mbunge wa Taveta na mwanasiasa mkongwe wa Taita, Marsden Madoka kuhama chama cha ODM hadi upande wa serikali, ilikuwa ni kuwepo na makubaliano ya kufalsafa kwamba Granton Samboja awanie kiti cha ubunge wa Wundanyi kutokana na ishara ya aliyekuwa mbunge Thomas Mwadeghu kuhakikisha kwamba atabana cheti cha ODM kwa ugavana.

Danson Mwazo ambaye wakati huu ameangukiwa kuwa mwenyekiti mpya wa shirika la huduma za feri nchini (Kenya Ferry Services-KFS), alijua nafasi ya ugavana kwa tikiti ya ODM hatoweza kufaulu na hatimaye akajua kwamba msukumo wa Madoka na Shaban utazaa matunda kupewa tikiti ya Jubilee kwa uchaguzi wa 2017.

Ili kuhama kutoka upinzani, Mwazo alitoa masharti ikiwa ni pamoja na hakikisho kamili la cheti hicho. Hakikisho kwamba mgombeaji wa Jubilee kwa ugavana wa Taita Taveta bila shaka unamwangukia Mwazo 2017, wafuasi chungu nzima wa kaunti ambao wamekuwa wakimpigia tebe Uhuru Kenyatta na William Ruto yadaiwa hawakufurahia na ndioposa wengine wakamsukuma Granton Samboja kuachana na wazo la ubunge wa Wundanyi kuburutwa kwa ugavana.

“Hata yeye mwenyewe hakuamini wakati ametangazwa kuwa ndiye gavana wa Taita Taveta ishara kamili kwamba hakuwa amejipanga. ASri yake na ambayo angeweza vyema, ilikuwa ni nafasi ya ubunge wa Wundanyi, ni kweli hakuwa anafi kiria urefu wa kina cha ugavana,” azungumza mkazi wa kaunti ambaye hakutaka jina lake litajwe.