Sambamba na sakata ya ‘Brexit’ ya Uingereza kujitenga jumuiya ya Ulaya ‘European Union’ (EU) yamkini Tanzania inajitia katika mwiba huo wanaojichoma waingereza.
Tukitathmini kwa kina mwenendo wa Tanzania katika swala zima la uwiano, umoja na maendeleo ya watu wa kanda hii ya Afrika Mashariki tunaona imekuwa kikwazo kikubwa kwa lengo hili nyeti.
Cha kushangaza ni kwamba mmoja wa waanzilishi wa jumuiya hii ni baba wa taifa hili yaani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Zaidi ya yote makao makuu ya jumuiya ya Afrika mashariki yalianzishwa mjini Arusha kule kule Tanzania na kudumu hadi leo. Akiwa na baba wa taifa la Kenya marehemu Mzee Jomo Kenyatta sambamba na Rais Milton Obote walianzisha umoja huu wa kanda.
Hatahivyo ndoto ya muungano thabiti wa Afrika mashariki umetatizwa na majirani wabongo kaka blaza kwa sababu tutakazobainisha hapa.
Kizungumkuti ni kwa Tanzania kuwa na woga na Kenya kwa kuona kuwa watamezwa kiuchumi na jirani alopiga hatua
kubwa za uchumi na siasa. Kimsingi ni wivu wa kuona maendeleo ya Kenya unaowazuzua watanzania.Tatizo hili lilianzishwa na Nyerere mwenyewe aloshindwa kuinuwa taifa lake kiuchumi alivyofanya Jomo.
Kivipi?
Nyerere alisoma na kupata elimu ya juu ya chuo kikuu maarufu kule Scotland cha Edinbourgh katika masomo ya siasa na uchumi. Sasa badala ya kutilia mkazo elimu na kuanzisha msingi kwa wananchi wake alipiga
mbiyu ya kuendeleza Kiswahili kwa umoja wa nchi.
Changamoto ya maendeleo
Je, itawezekana vipi kuboresha watu wasio na elimu hususan kiuchumi? Ni kweli Kiswahili kimeondosha ukabila na
kuleta mshikamano wa mtanzania lakini bado wamesalia ujingani katika karne hii ya teknolojia.
Nyerere wa kabila la kizanaki kutoka kijiji cha Butiama kule Bukoba, alisomeshwa na wamishonari kidini na kielimu.Mbona hakutaka watanzania wasome kama yeye? Kunapofuka moshi kuna moto. Nyerere alihofu watanzania
wakisoma wataerevuka na kutisha uongozi wake.Alitaka wawe wajinga ili awatawale na kuwazuzuwa Nyerere alifaulu kwani watanzania mpaka leo wanamuenzi.
Stay informed. Subscribe to our newsletter
Twakumbuka nyimbo fulani ya kale kule bongo inayojumuisha mapenzi mazito ya wabongo kwa Nyerere. Mistari ni hii:-
“Ndugu Juliasi Kambarage Nyerere si kwamba yeye tu….ni kiongozi halisi…bali pia ni mwalimu.. alo na kipaji cha ukarimu…. Na hakuna asiye mfahamu…anayeshirikiana nasi katika shidana raha...”
Kimsingi Nyerere aliwateka akili watanzania kifikra akitumia masomo ya kifalsafa na siasaalosoma kule Edinbourgh.
Nyerere mjanja alianzisha siasa za ujamaa na kujitegemea na kuwarundika watanzania katika ufukara wa ukulima wa
kikale. Aliogopa kukuza wasomi bali alitaka wajinga kuwaongoza. Aghalabu alizinduwa azimio la Arusha kama sheria kuu ya kikatiba.Akifuata siasa za kidikteta na za kiimla za Mao Tse Tung wa China, Nyerere alisuta ubepari kabisa asijuwe kuna nukta fulani nyeti katika mfumo huu ambao Kenya walifata.
Malumbano
Nyerere katika kilele cha uhasama na Kenya alitaja Kenya kuwa jamii ya mtu kula mtu mwenzake. Akimjibu Kenyatta kwa kuiita Tanzania nchi ya mtu asiyekula chochote! Nyerere mwenywe alikiri mwishoni mwa awamu yake kuwa ujamaa haukuleta ufanisi kama kwanza alofikiria.Alijidanganya kuwa Tanzania ingekua ama Uchina asijuwe uchanga wa taifa lake ukilinganisha na China pevu.
Matokeo yake watanzania walifukarika wakawa madutu na washamba wakiwa ndani ya nchi tajiri ya raslimali sufufu lakini bila ya wasomi na watalamu wakugunduwa na kukuza. Huku Nyerere akilemaza watanzania Jomo Kenyatta aliendeleza elimu kwa wakenya akisisitiza matumizi ya kiingereza kama lugha ya kimataifa na kiuchumi.
Kenya ilpiga hatuwa huku vijana wakisoma kwa bidii wakati watanzania wakipepeta kiswahili kule katika vijiji vya ujamaa na kujitegemea.
Nyerere aliboresha udikteta wa chama kimoja cha TANU kisha cha mapinduzi (CCM) ikifata mfumo wa Uchina.
Wakiwa bila ilimu ya fikra watanzania walimuabudu Mwalimu aliyekuwa akiwachekesha kwa hotuba zake za mahanjam na uchali zilojaa inadi, sitiazai na hekaya za Abunuasi. Kenya ilipiga hatua kubwa kiuchumi na
Nyerere alifahamu hili na hata kuitambuwa Kenya kama nyota ya jaha na hata kujisahau na kuitaja katika hotuba zake.
Mfano dhahiri ni pale vijana wengi wa Tanzania walivyotaka kwenda nje ya nchi kule Ulaya na Marekani kwa masomo na makazi kama wenzao wakenya walivyosaidiwa na serikali yao. Nyerere alipochoka na kerohili aliwaambia watanzania hao hivi (nukuu):-
Ulaya iliyo Afrika
‘Uraya (ulaya) yanini? na uraya iko hapa hapa jirani (Nairobi)!.. nendeni hapa uraya !’alisema huku kama kawaida
yake akishangiliwa kwa nderemo na vifijo naye akihitimisha kwa kicheko chake kirefu cha gugumizi’ hee..hee..heee!’
Nyerere ambaye alibarikiwa kwa kuzungumza kwa haraka kama cherehani ya stima aliheshimiwa kupita kiasi na jibulake kwa swali lolote lilichukuliwa ukweli mtupu na hakuna wakupinga kwani baba kasema!
Viongozi wa chama tawala cha CCM kama Ngumbare Mwiro, Rashid Kawawa na kina Abeid Jumbe walishikilia sera za mwalimu kikamilifu na kuzitekeleza. Marais waliofuata kama Benjamin Mkapa, Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Mrisho Kikwete na kwa kiasi fulani wa sasa John Pombe Magufuli walifata sera za Mwalimu. Aghalabu mfano wa m’buyu mkongwe ilikuwa kazi kung’owa kabisa mizizi ya ujamaa alozika Nyerere katika ardhi ya Tanzania.
Twaweza kusema Kikwete ambaye alikuwa kiongozi kijana wakati wa Nyerere alifuzu sera na hata tabia za babu yake huyo.
Alipokuwa Rais Kikwete alitawala kama Nyerere na kuzidi kulemaza Tanzania hususan kiuchumi
kwani ufisadi ulizidi kukithiri huku yeye akichekacheka tu! Kikwete alipenda sana kusafirinje ya nchi kwa kigezo cha kusoma mambo ya nchi ziloendelea.
Kuna wakati alitembelea Uhispania na kwende katika uwanja wa timu maarufu ya soka Barcelona kule Camp Nou. Aliporudi Tanzania aliisifu uwanja huo wa mpira ulivyopendeza eti ni mzuri!
Ni wakati wa Kikwete Tanzania ilipojitenga kwa muda na jumuiya ya Afrika mashariki na kujiunga na umoja wa kusini
mwa Afrika yaani SADEC.