Wale ambao walikuwa wafuasi wa minenguo ya rhumba na chakacha katika miaka ya mwanzoni hadi miaka ya 1990s, bila shaka jina la Princess Farida kwao silo geni. Farida ambaye alililipata jina lake hili kwa ushindi wa miaka mfululizo katika mashindano ya mnenguaji wa dansi ya “Chakacha”, miaka ya tisini, amekuwepo ulingoni mwa muziki kwa zaizi ya miaka 20 na hivi ametoka jikoni na kibao kipya cha Ra? ki wa Kweli kinachofuatia kingine kinachoendelea kubobea cha Amelipa.
Hapa amemshirikisha mwimbaji mwingine hodari kwa midundo ya kikamba, maarufu tu kama Ndilima. Malkia wa Chakacha Jinsi alivyopepengua kiuno kwenye ngoma ya chakacha, kamwe haungesita kuivunja shingo yako kadiri msukumo wa ngoma na dansi yake inavyokupeleka.
Princess Farida alikuwa bingwa wa mashindano ya kitaifa ya msakataji mashusi wa chakacha na hivyo wengi kumdhania kama siyo toto la ‘Kidigo’ basi labda kipusa cha mchanganyiko wa Mshelisheli na Mswahili. Ijapo Farida alizaliwa katika mitaa ya Majingo, kaunti ya Mombasa, wazazi wake wako na mizizi ya ukambani na wameinukia jijini Nairobi. Waliokuwa hawasikii wala kuona juu ya muziki miaka hiyo ya tisini na ambao bado wapenzi wa minenguo hiyo, tuna uhakika kwamba bado wanamkumbuka vyema akiwa sakafuni akibingirisha chakacha na hatimaye kukuza kipawa chake cha uimbaji aliposhirikiana na makundi mashuhuri ya Nairobi na Kenya yaThem Mushrooms na Bora Bora Sounds miongoni mwa makundi mengine kabla ya kuanzisha kundi lake na kuamua kuokoka na kubadili uimbaji wa injili hadi leo.
Yamebakia mjango Mambo ya kutingisha dansi ya chakacha kwake yalibakia ya mjango tu tangu mwaka 2001 alipoamua kwamba ni wakati wa kumtumikia Mungu wake kwa kuokoka na kubadili mienendo yake ya kimuziki kutoka muziki wa dansi hadi wa injili.
Kwa wafuasi wa nyimbo za injili na Wakristo wanaothamini kipawa cha mwanamuziki, watakubaliana nasi wakati wakisikiza kibao chake kipa cha Amelipa ambacho kimeporomoshwa kwa lugha sanifu ya Kiswahili kinachozungumzia masuala muhimu ya msimu huu wa pasaka.
Licha ya wafusi wa miziki ya injili na kwa kuwa muziki hauna mipaka ya kikabila wala lugha, wapenzi wa nyimbo za taarabu na misakato ya chakacha hali kadhalika watafurahia siyo hapa wakati wanaposikiza kibao chake kipya kwani kimepikwa kwa mchanganyiko wa uhondo wa mapigo ya chakacha na ile ya taarab. “Mpangilio wa nyimbo hii nilinuia kuwaleta karibu wafuasi wangu wote wanaonifahamu kwa chakacha na waumini wenzangu na mashabiki wangu wa nyimbo za injili ili kuhakikisha kwamba ujumbe wote wa Mungu umem? kia kila mmoja.
“Hii ni baada ya kugundua kuwa miongoni mwa wasanii wenzangu hubwagiza nyimbo siyo kwa madhumuni ya kuwalenga na kurekebisha tabia za wale waliopotea bali kwa lengo la biashara na umaarufu wao wenyewe.” Azungumza Farida. Farida ambaye anajivunia kubarikiwa kuwa mama na mke anayefurahia maisha ya familia yake (mzazi), mtunzi, mshauri wa masuala mbali mbali yakiwemo ya kijamii, kielelzo kwa wasanii wengine, amerekodi jumla ya santuri (album) kwa chapa chake mwenyewe.
“Nimeamua kuchomoza kibao hiki ambacho licha ya kuwa kimesakatwa kwa ujumbe wa kiinjili, bado kinawakumba wafuasi wa miziki ya kawaida, ni kuhakikisha kwamba nimewaleta karibu mashabiki wote, wale waliookoka na wale ambao wamekuwa wakisubiri kuraiwa kuja kwa ukombozi wa bwana,” aongeza mwimbaji wetu Farida, Ziara ya Marekani Mwanamuziki Princess Farida amerejea hivi juzi nchini baada ya ziara yake ya miezi mitano ya Marekani ambayo ilimtembezwa zaidi ya maeneo (states) 20 ya nchi hiyo ambapo alitumbuiza majukwaa tofauti ya burudani la injili pamoja na mahubiri mbali mbali ya kueneza jina la Bwana. Kulingana na Farida, pia alitumia fursa hii kuvitembelea vituo vya habari tofauti vya Marekani kwa jitihada za kutangaza mahibiri yake.
Akizungumzia siri yake kama msanii aliyebobea kwa miziki ya dansi na injili, Farida anawashauri wasanii wanaochipuka kwamba wakati unapokuamua kuimba ujumbe wa Mungu, unatakiwa kuwa mjumbe wake kwa kuzingatia maudhui mahsusi ya kueneza injili kwani hata wadau mara nyingi hukupa heshima ya kipawa chako kuambatana na msimamo wako wa talanta. “Uimbaji siyo tu kuamka na kuimba bila malengo. Unapoimba, imba maudhui yenye mafunzo na
maandiko yanayoweza kumgeuza mtu kiroho ama kutoa wusia mwema kwa jamii. Utunzi unahitaji kipawa na wakati mzuri wa kupiga msasa kazi yako,” ashauri msanii Farida ambaye anasema kuwa bila kujizatiti hivyo kama msanii, huenda ukawa mashuhuri wa muda kabla ya kuyeyukia kaburi la sahau la umaarufu wako.
Farida anasema kuwa msanii wa injili na yule wa dansi ya kawaida wanaweza kushirikiana kwa lengo fulani na wakato nyimbo mradi tu unawasaidia kuwagusa nyoyo mashabiki wa pande zote mbili. Anasema katika ulimwenguni kunao ufalme mara mbili, wa usiku na mchana ambao kusema kweli hakuna siku unaweza kushikana ama kuchanganyika. “Hakuna njia ya usawa inayotumiwa na vitu hivi viwili ni aidha uwe unamtumikia Mungu ama uwe unamtumikia shetani. Mungu hana utani na huwezi kumfananisha” anahubiri maneno ya uzito kwa kiasi. Uandishi vitabu Alipata motisha wa kuandika vitabu punde tu alipopata fursa ya kuhojiwa katika kipindi mashuhuri cha runinga chenye mkondo wake nchini Marekani cha America’s Club 700 CBN.
mnamo mwaka 2014. Hatimaye alipata mialiko zaidi katika vituo vinginevyo vya kimataifa kutoa ushuhuda wake wa maisha yake ya awali na uzaliwa wake mpya. Yaaminika ni kupitia kwa mahojiano ya Club 700 CBN ambapo maonyesho yake yalisambazwa katika lugha mbali mbali ulimwenguni (tafsiriwa) na kuzoa umaarufu siyo haba. Kitabu chake cha kwanza kilikuwa cha The New Me (chenye kumaanisha “Ni Mimi Mpya”) ambacho kinasumulia maisha yake kutoka ya kuruka majoka (madisko) hadi kubadilika na kujiosha upya na muosho wa injili. Kitabu chake cha pili kinafahamika kama Princess Gems Every Girl Should Have ambacho kwa urahisi wake kina maanisha “Mbinu za Malkia ambazo kila
msichana anastahili kuwa nazo” ambacho kinaelezea jitihada zake kama msichana kutoka nyakati zake za utotoni hadi mahala alipo? kia sasa kimaisha. Kitabu cha Princess Farida cha tatu, kinajulikana kama Power of the Tongue ama kwa lugha ya kitaifa, “Nguvu za Ulimi ama Maneno” hapa akizungumzia jinsi ya kurekebisha mawazo ya wasanii ambao hubobokwa tu nyimbo ambazo hazina malengo mema ama kumlenga Mungu kuambatana na mawaidha yake kwa umma.
Nani kama mama Princess Farida ni mama kama wengine ambaye licha ya shughuli tele hizi, kamwe hawezi kuepuka majukuma yake kama mama na mke. Anao watoto wake wawili Shekaina na Hadasa huku mwaka huu akisherehekea miaka 13 tangu kufungua ndoa chini ya uwezo wa Mungu kama mlinzi na mwenye kukinga ndoa yake kama anavyosimulia. “Yashangaza kwamba kunao baadhi ya watu ambao bado wananidhania kuwa mimi ni yule Farida wa zamani ilhali sivyo. Wanaume wengine wangali wakitaka kuona nikinenua chakacha hali ambayo haiendi sawa na maamini yangu leo. Hawajui kwamba mimi ni Mkristo kamili na niliyefunga ndoa,” agusia misukumo ya wanaume wengine ambao ni wanaadamu lakini roho zao za ma? si.
Stay informed. Subscribe to our newsletter
Hatahivyo ana? chua kuwa licha ya dada zake wawili kuungana nao kwa kuokoka kwa jina la Yesu pamoja na mama yao mzazi, isipokuwa Baba yake na kaka yake mdogo mashuhuri pia kwa muziki na maarufu kwa jina la misakato kama Kanda King (miaka ya 1990s pia alifahamika kama Kanda Kid akiwa mcheza dansi maalum la Kwasa Kwasa kabla ya kugeuza King alipoanzisha bendi yake mwenyewe) wakiwa ni Waislamu.
Princess Farida alizaliwa Mvita, Mombasa na kubobea kwa kuwa malkia wa dansi ya chakacha hadi kuwahamisha wazazi wake kutoka Mombasa hadi Nairobi miaka ya katikati mwa 1990s. Hatimaye alizoa umaarufu zaidi na kuzuru mataifa chungu nzima ya kigeni na hususani kuwa na makao mjini Dubai ambapo alitumbuiza watu wa tabaka tofauti wakiwemo Marais wa nchi mbali mbali na kadhalika. Hali kadhalika ameshiriki katika makundi ya wanamuziki maarufu duniani akiwa Dubai n ahata kuzuru kwingineko akiwa na wanamuziki mashuhuri wa humu nchini Them Mushrooms wakiongozwa na Teddy Kalanda Harrison na ile bendi ya mkongo maarufu ya Koffi Olomide akiwa pamoja na mdogo wake Kanda King wakiwa wasakata densi na kuchangia uimbaji.