Vijana washirikiana kupambana na vita dhidi ya mihadarati

Loading Article...

For the best experience, please enable JavaScript in your browser settings.

Viongozi wa vijana kutoka mashirika mbali mbali ya kijamii katika kaunti ya Mombasa wakijumuika pamoja na Mhariri mtekelezaji wa gazeti la Pambazuko baada ya zoezi la kuwapa motisha katika kukuza talanta zao kwenye ukumbi wa kijamii wa uhamazishaji wa mikoko wa Comensum ulioko wadi ya Bamburi kaunti ndogo ya Kisauni, Mombasa.

Vijana kutoka kaunti ndogo sita za Mombasa zinazojumuisha Kisauni, Nyali, Mvita, Likoni, Changamwe na Jomvu wameungana kupitia kwa muungano wa mashirika ya kijamii kuhakikisha kwamba hakuna muda unapotezwa na kijana yeyote yule kama njia mojawapo ya kupambana na ugaidi na utumizi wa mihadarati.

Wakiongwa na James Ruwa na Omar Chai wanatoa wito kwa washikadau wa kaunti kuwasombeza vijana katika kuwapa nafasi ya kujiendeleza siyo tu kimawazo ya masomo bali kuwasumuka katika kuona kwamba talanta zao zimeimarika.

Ruwa na Chai walitoa changamoto walipokuwa wakitamatisha mafunzo kwa vijana katika uhifadhi wa mikoko, mbinu za kuimarisha talanta za usanii wa muziki, uchoraji, mavazi na mapambo, filamu, usemaji wa hadhara (Public Speaker), uhifadhi wa mazingira na jinsi ya kuishi vyema na majirani katika jamii kwenye ukumbi wa kijamii wa Comensum Research Centre ulioko ufukwe wa Majaoni, Bamburi kaunti ndogo ya Kisauni.

Waendashaji wa vikao hivyo vya siku tatu, James Ruwa aliwakilisha shirika la Green String Network ilhali Omar Chai alikuwa kinara mwakilishi wa Kadzandani Creative Youth. Wengi waliofanikisha mafunzo hayo ni wasanii mbali mbali ambao waliondoka na azimio la kumrekebisha kijana yeyote yule wa Mombasa nan chi nzima kwa jumla.

Viongozi na waekezaji wameombwa kusaidia kukuza jitihada za vijana wenye bidi kama hawa na wakati huo huo wakuu wa serikali kushauriwa kuwashika mkono katika mikakati ya kudumisha usalama mashinani na kampeini za kulinda mazingira na kupambana na janga la matumizi ya mihadarati kwa vijana.

Msimamizi wa ukumbi huo Daniel Taura anasema kuwa amefurahishwa na baadhi ya vijana ambao wamejitolea na kujitoa mhanga wa kuwafunza wenzao mambo ambayo wangetumia pesa kwingineko kufunzwa. Ingawa hivyo anashinikiza wizara za utalii, elimu, idara ya usalama wa ndani, mazingira na teknolojia katika ngazi za kaunti na serikali kuu kupiga jeki za vijana kama hawa.

Ukumbi wa Comensum RC unao uwezo wa kuendesha kikao cha watu zaidi ya 100 kwa pamoja, ukiwa na sebule ya kando ya mkahawa mdogo ambao wageni wanaweza kujivinjari wakati wakipumua kwenye mikutano yao. Changamoto hata hivyo ni ukosefu wa maji masafi na muundo msingi wa njia nzuri licha ya kuwa ni kivutio halisi cha utalii.

Taura anasema shughuli zao ni kupanda mikoko, kuhifadhi mazingira na wakati huo huo wakianza miradi ya kutega na kufuga makaa ya baharini.