For the best experience, please enable JavaScript in your browser settings.
Kungamano ililosimamiwa na rais Obama pamoja na marais kutoka Kenya, Uganda na Ethiopia na mawakilishi wa Riak Machar na Salva Kir ni nafasi ya mwisho kupata suluhu kwa janga na maafa ya vita vilivyoikumba taifa la Sudan Kusini. Bwana Obama amedhihirisha bayana kwamba kama mazungumuzo hayatapata mafanikio, basi hakutakuwa na njia nyingine isipokuwa kuwawekea mahasimu hao vikwazo vya kiuchumi.
Mbarika ya Sudan Kusini ni donda ngumu kuponya. Kunayo changamoto tofauti zinazoungana pamoja kuzorotesha hali ya usalama huko. Jambo la kwanza ni kutapakaa kote Sudan Kusini kwa silaha ndogo kwa ajili ya miaka mingi ya vita nchini humo. Itabidi jamii ya kimataifa ipate njia ya kuzuia uagizaji wa silaha nchini humo.
Pia kuna swali la majeshi ya Uganda nchini Sudan Kusini yanayomuunga mkono Bwana Salva Kir. Majeshi ya Uganda yanazorotesha uwezekano wa upatanishi kwa sababu upande wa Riak Machar unadai majeshi haya ni majeshi ya kigeni na hayapaswi kuwa Sudan Kusini.
Jambo la tatu kuu ni rasilmali ya mafuta inayopatikana kwa wingi kwenye eneyo inayokaliwa na majeshi ya Bwana Machar. Hii ndiyo changamoto inayofanya waasi wa Bwana Machar kuendelea kupigana. Wanataka kushikilia eneo hii kwa sababu ya mamia ya mabola wanazozipata kwa kandarasi zinazotolewa kwa kampuni za kigeni. Pia wanafaidika kwa kandarasi za utafutaji wa mafuta na malipo ya kulinda wachimba mafuta hayo. Isisahaulike kwamba serekali ya Sudan Khartoum haijawacha kuzorotesha hali ya usalama Sudan Kusini kwa kuwapatia waasi silaha. Mwishoe, itabidi madola makubwa kama Uchina, Marekani, Urusi na Uingereza kushinikiza Umoja wa Mataifa kuipachika Sudan Kusini na vikwazo vya kiuchumi.
Jitihada za bwana Obama zinachangia kwa mzozo wa Sudan Kusini kuangaziwa taa kwenye janga la mizozo tofauti duniani kote. Itabaki kwa viongozi wa nchi hio kupata jawabu kwa mzozo huu wa kisiasa na kibinadamu. Obama anaweza kupatanisha pande zote mbili pekee.