Je ni sahihi kuteua Museveni kuwa mpatanishi mkuu Burundi?

Loading Article...

For the best experience, please enable JavaScript in your browser settings.

Hivi karibuni, jumuia ya Afrika Mashariki ilimteua Rais Yoweri Museveni kuwa mpatanishi mkuu kati ya serekali ya Pierre Nkurunziza na mahasimu wake. Hali tete Burundi ilizoroteka zaidi wakati mwasi mmoja mkuu bwana Godefroid Niyombere, alisema katika mahojiano na stesheni ya KTN kwamba wakosoaji wa serekali ya Nkurunziza wameamua ni vita pekee vitakavyo weza kutatua mbarika ya kisiasa Burundi.

Changamoto zilizoikumba Burundi zilidhihirika wazi wakati bwana Nkurunziza alipowania hatamu ya tatu kwenye uchaguzi wa urais. Jumuia ya Afrika Mashariki iliyokutana Dar es Salam jumatatu wiki hii ilipendekeza kuahirisha uchaguzi wa rais kwa wiki mbili kutoka July 15th hadi July 30th 2015.

Wanadiplomasia wanatabiri ya kwamba wakati huu utatumiwa kufanya majadiliano kati ya serikali ya Burundi na upande wa upinzani. Inaonekana kwamba bwana Nkurunziza amepuuza azimio hii kwa kuendelea na heka heka zake za kampeini kutafuta awamu ya tatu. Dosari iliyopo kwenye azimio ya Dar es Salam ni kwamba haijashugulikia swala la awamu ya tatu kwa bwana Nkurunziza.  

Haya yote yakiwa vile yalivyo, haionekani kwamba upande wa upinzani utakubali msimamo wowote itakayomruhusu Nkurunziza kuendelea madarakani kwa awamu ya tatu. Kwa sasa, hali ya patashika iliyopo Burundi inaonekana itaendelea kwa muda mrefu. Nafasi ya kupanua uhuru wa kisiasa nchini humo umepita. Kwa sasa, inaonekana kwamba donda hii ya kisiasa itatatuliwa kimabavu na mahasimu waliopo Bujumbura.