Karisa Maitha ndiye chanzo cha kina Joho kutajirika

Gavana Hassan Joho.

Wanaoitika wafalme wakikohoa kamwe siyo wafuasi wa kanisa la Neno Evangelism Centre la Pasta James Nganga pekee bali kunao wangwana wengine mashinani ambao wakiteuka tu, wengine hupaparika kuitika hewala bwana!

Kabla ya kuchipuka kwa familia ya Joho, ikiongozwa na nguzo ya kaunti ya Mombasa na pwani nzima kwa jumla ya misingi ya kisiasa Abubakar ‘Alpha’ Joho hadi kufikia 2004, Mgongo wa pwani, marehemu Emmanuel Karisa Maitha ndiye aliyekuwa aking’orota vinyabwela (makalameni) wote wa kisiasa walikuwa wanaingia mwituni.

Karisa Maitha kama tulivyoweza kumzungumzia kaatika matoleo ya awali, alikuwa kiongozi mcheshi lakini haba kwenye ulingo wa kibiashara.

Kama kawaida ya wanasiasa maarifa ya biashara. Siku moja mnamo mapema mwaka 2003, aliwaita kwa kumtuma mmoja wa madereva wake kuwachukua Abu na Hassan kuja kuwaonyesha mtu ambaye angesaidiana nao katika kuvunja nyuta za milango ya kutafuta biashara wakati wa serikali ya Kibaki. “Mimi nilitumwa na mheshimiwa Maitha kwenda kuwachukua mheshimiwa gavana Hassan Joho na kakake mkubwa Abubakar na wakati nilipowafikisha hotelini nikamkuta mzee amekaa na Mary Wambui ambaye pia hakuwa mgeni kwangu kwani nyakati zote za kampeini ya DP za pwani, daima alikuwa anaambatana na Rais mstaafu Kibaki na Maitha,” azungumza mmoja wa madereva wa marehemu Maitha ambaye kwa sasa ameajiriwa na kampuni za kibinafsi. Mkono wa Wambui Wadadisi wa siasa wanasema kwamba Karisa Maitha alitaka kuinua vipawa tofauti vya biashara mbali na wafanya biashara mashuhuri ambao walikuwa wakimfuatafuata kwa usaidizi wa kupata nafasi za kandarasi za serikali. Inadaiwa ni kutokana na mkono wa Karisa Maitha kuwaunganisha vigogo wa leo pwani hususan Abubakar ‘Alpha’ Joho na gavana wa Mombasa Hassan Joho.

Baada ya kujulishwa kwa Mary Wambui, ndugu hawa wawili mashuhuri walibobea kwa kuanza kutumia vyema fursa hiyo kuanza kupata zabuni kupitia kwa kampuni yao ya Prima kabla ya kusajili nyinginezo chungu nzima na kujihusisha kupanua biashara zao katika kila nyanja.

Hali ilikuwa nywee hadi pale Karisa Maitha alipofariki ghafla akiwa ziarani nchini Ujerumani. Wakati huo, tayari walikuwa wameanza kuimarika kibiashara kutokana na mlolongo wa kazi ama zabuni walizofanikiwa kuzipata katika bandari ya Mombasa na idara nyingine za serikali kama neno la Karisa Maitha kuwasaidia kushikana bega kwa bega kibiashara na wakaribu wa Kibaki. Awali kabla ya kushikwa mkono wa kheri na Maitha, Abu alikuwa anamiliki kampuni miaka ya nyuma ya huduma za bandarini maarufu kama Say Enterprises ikiwa na afisi yake katika chungu nzima wa pwani, pato lao jingi huwa ni la kula tu wala siyo kujiwekea kutokana kwamba mtu mmoja huwa ni mlezi wa familia nzima. Hii ni kawaida ya umaskini wetu. Mkutano wa Maitha Hadi mwaka wa 2003, majina ya Abubakar ‘Alpha’ Joho na nduguye Hassan Joho kamwe yalikuwa hayapo kwenye ulingo wa biashara zilizokita. Ingawa hivyo, bidii yao kikazi ilikikuwa imemgusa Mgogo Karisa Maitha ambaye alikuwa amebahatika kupata uwaziri kwa serikali ya nusu mkate ya Mwai Kibaki na Raila Odinga.

Kwa kuwa alikuwa mkaribu sana na Rais Mwai Kibaki, Maitha aliwaza ni njia gani anaweza kuwatafuta vijana wenye ari ya biashara na ambao wanaweza kubobea mradi tu waonyeshwe njia. Kupitia kwa jamaa wa familia ya karibu na ile ya kina Joho, Yusuf Mkali ambaye Maitha alimjua kwa muda kama mwanabiashara, kaka hawa Abu na Hassan Joho hususan Abu ambaye amechangamka kibiashara kwa muda, walipata afueni ya kukutana na Maitha kwa mijadala zaidi ya kibiashara. Urafiki wa karibu Kulingana na wakaribu wa marehemu Karisa Maitha na wale wa familia ya kina Joho, inabainika kwamba Maitha aliwahusudu sana Abu na nduguye kutokana na bidii na Enterprises ikiwa na afisi yake katika barabara ya Jomo Kenyatta karibu na shule ya magari ya AA Driving, Mombasa.

Balozi wa Jamhuri ya kitaifa ya Qatar nchini Jabr Bin Ali Al-Dosari alipomtembelea Abubakar Joho alipozuru Mombasa. Walimkuta Alpha akiwa na magavana wawili Granton Samboja (Taita Taveta) na Dhadho Godhana wa Tana River. Alpha ndiye mwenyekiti wa Wakfu wa Joho Foundation.

Kampuni hii ya Say Enterprises walibadilisha umilikiaji wake kutoka kwa wakurugenzi wa kwanza Mzee Shirazi na aliyekuwa kama meneja mshikilizi Yusuf Mkali ambaye pia ni mkaribu wao katika familia. Ushupavu wa Abu ulianzia hapa kwa Say Enterprises na anajua ni heshima gani bado anamuenzi nayo jomba Yusuf Mkali kwa kumfungulia njia hii ya biashara.

Uchaguzi wa Kisauni 2005 Uachguzi mdogo wa eneo bunge la Kisauni wa mwaka 2005 ambao ulitokana na kifo cha Maitha, ulimtambulisha rasmi Hassan Joho na kakake Abubakar kwa umma wakati alipotumia zaidi ya kitita cha shilingi milioni 34 kwenye uchaguzi huo mdogo. Ni mwaka huu ambapo wengi walimjua ‘Alpha’ kwamba ni moto wa kuotea mbali katika maswala ya mipangilio ya kisiasa. Ijapo mshindi wa uchaguzi huu mdogo alikuwa ni Anania Mwaboza, Balozi wa Jamhuri ya kitaifa ya Qatar nchini Jabr Bin Ali Al-Dosari alipomtembelea Abubakar Joho alipozuru Mombasa. Walimkuta Alpha akiwa na magavana wawili Granton Samboja (Taita Taveta) na Dhadho Godhana wa Tana River. Alpha ndiye mwenyekiti wa Wakfu wa Joho Foundation.

Mama Mary Wambui aliyekuwa mbunge wa Othaya. Yeye ndiye aliwasaidia kina Joho kubebea kibiashara.

Twaarifiwa kwamba hata kile kitendo cha serikali kuchoma kiwango kikubwa cha sukari maeneo ya Mwakirunge, Kisauni na vituko vingine vya kumkanyagia gavana Hassan Joho, ilitokana na hamaki za kukorofi shana kwa muda na utawala wa Uhuru Kenyatta. Mcheshi ‘Alpha’ Muda wote huo, mahiri wa biashara pwani na mlezi wa wanasiasa wengi kuanzia Vanga hadi Kiunga, Abu alikuwa akicheza ukubwa wa jaa kwani kila mara alikuwa gavana Joho akiharibu serikalini, yeye ndiye aliyekuwa akibambanya uhusiano wao na serikali uwe sawa kwa sababu ya biashara. Yeye na siasa ni pamba na moto lakini ndiye mwenye kujua nani anaweza kufaulu wapi kiuongozi.

Leo hii Abu amefi kia kiwango cha kutegemewa na wengi siyo tu wanasiasa wa pwani na majimbo mengine nchini bali hata wananchi wa kawaida. Wanamchukulia kuwa miongoni mwa roho nzuri anayefananishwa na Karisa Maitha peke yake katika masuala ya kusaidia. Akiwa mwenyekiti wa Wakfu wa Joho Foundation ameweza kupanua mbawa zake za kisiasa na biashara siyo barani Afrika tu lakini hadi ng’ambo katika kona zote za bara ulaya. Nguzo ya wanasiasa Yaaminika leo hii, ndiye nguzo ya wanasiasa wote kuanzia wawakilishi wa wadi hadi magavana na wala hakuna gavana wa chama cha ODM ambaye anaweza kuyumbayumba mbele yake. Wabunge karibu wote katika uchaguzi mkuu wa 2007, 2013 na 2017 walipata msaada wa aina moja ama nyingine kutoka kwake.

Ukarimu alionao, umewasaidia vijana wengi kikazi na yaaminika kwamba licha ya kuwa mmoja wa matajiri wakubwa nchini Kenya, yeye yungali akiishi katika mazingira ya kawaida huku marafi ki wake chungu nzima wakiwa ni vijana mitaani na masikani yao kama zamani.

Takribani ya vijana chungu nzima wa kaunti ya Mombasa, wanamwiita ‘Boss’ kutokana kwamba masomo, kazi na kodi yungali akiwasaidia licha ya madeni ya hospitali kuu ya mkoa ya Coast General kwamba anayalipa kila mwezi kwa wagonjwa zaidi ya 50 wanaoshindwa kulipa matibabu yao.

Hekalu ya 2022 Ingawa hivyo, wadadisi wa siasa ya Mombasa wanajiuliza iwapo nguvu za familia ya Joho zitathibiti mawimbi ya mabadiliko ya kisiasa na uongozi yajayo katika uchaguzi mkuu wa 2022? Kwanza Rais Uhuru Kenyatta anaelekea kukamilisha kipindi chake na haijulikani ni nani ataingia baada yake. Ganava wa Mombasa naye Hassan Joho anaondoka 2022 na bado haijafahamika nani anaweza kumrithi baadaye. Wengi twasubiri ngoma hii ya ukayi baada ya 2022.