Ulanguzi wa binadamu sasa wajitokeza Kenya

Afisa wa polisi akiwa na mshukiwa mmoja wa ulanguzi wa binadamu, Nakuru. [Picha: Standard]

Biashara ya ulanguzi wa binadamu yaonekana imechukua hatua nyengine baada ya tekinologia ya kisasa kuhusika pakubwa katika kufanywa kwa biashara hiyo haramu ya wanadamu.

Utandawazi bado ndio kigezo kikuu kwa shuguli za ulanguzi wa binadamu katika eneo la Afrika mashariki na kati.

Kulingana na shirika ambalo linashughulikia wahanga wa biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu la Trace Kenya, biashara hiyo imechangiwa pakubwa na utandawazi ikiwemo mitandao ya kijamii. Mkurugenzi wa shirika hilo Paul Adhouch amesema kuongezeka kwa biashara hiyo kumechangiwa na umasikini pamoja na hali ngumu ya maisha.

“Ulanguzi wa binadamu umekithiri sana na kuongezeka kwa sababu ya umasikini na mbinu ambazo watu hutumia kutafuta kazi katika mataifa ya nje. Mitandao imechangia pakubwa sana pia katika biashara hii,” akasema Adhouch.

Akizungumza katika mkutano uliowaleta pamoja waandishi wa habari ili kuangazia swala la ulanguzi wa binadamu, mkurugenzi huyo hata hivyo amesema vijana wengi wa kati ya miaka 20 hadi 29 ndio walengwa zaidi na kuathirika na mitego hiyo, huku asilimia kubwa ya wasichana wakitumika kwa biashara ya ngono.

Kulingana na Adhouch, eneo la Pwani hapo zamani lilijulikana kwa ulanguzi wa watoto wadogo, ikilinganishwa na wakati huu ambapo biashara hiyo imechukua mkondo mwengine wa kulazimisha watu wazima kufanyishwa kazi mataifa ya nje.

“Kwa muda mrefu sana hapa Pwani ulanguzi ulikuwa ni wa watoto kufanyiwa biashara, lakini sasa walanguzi wamekumbatia mfumo tofauti ambao watu wazima pia wanatumika kufanya kazi,” akataja Adhouch.

Wahusika wa biashara hiyo ya ulanguzi wa binadamu yadaiwa ni wakazi wa hapa Pwani ambao wanafaidi kwa kitita kikubwa cha pesa kutoka kwa walanguzi wakuu walio katika mataifa ya ughaibuni.

“Kitambo walanguzi walikuwa wanatoka ughaibuni lakini sasa hapa Pwani walanguzi wamekuwa wengine sana na wanafanya biashara hiyo haramu,” akaongeza.

Hata hivyo biashara hiyo mara nyingi imehusisha watu wanaoishi na ulemavu kutumiwa na kuwekwa katika maeneo ya katikati ya jiji la Mombasa na kuomba msaada.

Waathiriwa

Salim Hamis ni mmoja wa waathiriwa ambaye aliangukia mikononi mwa wakala ambaye anasema alihusika pakubwa na kujipata katika taifa la Saudia ambako anasema alifanyishwa kazi ambazo hazikuwa katika mkataba wa maelewano na wakala huyo.

Katika mkataba alioandikishiana na wakala wake alikuwa anaenda Saudia ili kufanya kazi ya udereva, hali ambayo ilibadilika na kuenda kufanya kazi ya shambani ambalo lilikuwa linasimamiwa na raia wa Yemen.

Hata hiyo Hamisi anasema alipitia mateso mengi pamoja na kukosa chakula, akisema kampuni ya mawakala ambayo ilmisafirisha ilimwambia atajisimamia kwa chakula.

Alilazimika kuacha kazi ya kuendesha Trella ambako alikuwa analipwa shilingi elfu hamsini na kuenda kufanya kazi ya shilingi elfu tisini mapatano ambayo hayakutimizwa na kuishia kulipwa shilingi eflu ishirini ambazo pia hakuzipata.

“ Nilitumia pesa nyingi hata mke wangu alichukua mkopo wa Kenya women kusudi niende nikafanye kazi ughaibuni, lakini hali haikuwa kama nilivyotarajia, nilipitia mambo mengi sana huko kufanya kazi ambayo haikuwa katika mkataba,”akasema Hamis.

Hamisi anasema alijaribu kutafuta usaidizi katika ubalozi wa Kenya nchini Saudi Arabia, lakini  ubalozi huo haukumsaidi na hata ukamwambia afadhali aendelee kufanya kazi pasipo kusikiliza kilio chake.

Anaushukuru ubalozi wa India ambao ulimsaidia katika kufanya juhudi za kurudi humu nchini ambapo alirudi kwa kutumia ndege inayotumika kubeba wakimbizi.

“Mimi ninavyosema ubalozi wa Kenya katika mataifa ya nje hausaidii kabisa. Unawapelekea malalamishi lakini hakuna msaada wowote unaopata. Ninaushuru ubalozi wa India ambao ulinisaidiakujinusuru kutoka Saudia Arabia,”akasema Hamisi.

Hamis anasema mawakala wengi wanaitumia fursa hiyo kuwalaghai watu na kuwaacha watu mikononi mwa watu ambao hawana ubinadamu bali kuwapeleka watu kwenye mateso katika mataifa hayo ya Ughaibuni.

Mizizi

Mwenyekiti katika kamati inayosimamia ulanguzi wa binadamu humu nchini Goerge Masese amesema hali hiyo imechangiwa na kupungua kwa makali ya sheria inayotakiwa kudhibiti biashara ya ulanguzi wa binadamu.

Masese amesema mara nyingi biashara hiyo inafanywa na viongozi wa tabaka za juu huku akisema hivi karibuni kamati hiyo itahakikisha kuwa sheria kali zinachukuliwa kwa wahusika ambao wanafanya biashara ya ulanguzi wa binadamu.

Mataifa ya Afrika ya kati, Bara Asia na Uropa yangali masoko makuu ya wahanga wa ulanguzi wa binadamu kutoka eneo la pwani ambao hutolewa viungo vya mwili na kuuzwa.

Ulanguzi umeweza kukithiri sana na kuongezeka kwa sababu ya umasikini na mbinu ambazo watu hutumia kutafuta kazi katika mataifa ya nje. Mitandao imechangia pakubwa sana pia katika biasharahiii,” akasema Adhouch.

Akizungumza katika mkutano uliowaleta pamoja waandishi wa habari ili kuangazia swala la ulanguzi wabinadamu ,mkurugenzi huyo hata hivyo amesema vijana wengi wa kati ya miaka 20 hadi 29 ndio walengwa zaidi na kuathirika na mitego hiyo huku asilimia kubwa ya wasichana wakitumika kwa biashara ya ngono.

Kulingana na Adhouch eneo la Pwani hapo zamani lilijulikana kwa ulanguzi wa watoto wadogo ikilinganishwa na wakati huu ambapo biashara hiyo imechukua mkondo mwengine wa kulazimisha watu wazima kufanyishwa kazi mataifa ya nje.

“Kwa muda mrefu sana hapa Pwani ulanguzi ulikuwa ni wa watoto kufanyiwa biashara lakini hali sasa imeingiwa na ulanguzi tafauti mwengine ambao ambao watu wazima pia wanatumika kufanya kazi,” akataja Adhouch.

Wahusika wa biashara hiyo ya ulanguzi wa binadamu wanadaiwa kuwa wakaazi wa hapa Pwani ambao wanafaidi kwa kitita kikubwa cha pesa kutoka walanguzi wakuu walio katika mataifa ya ughaibuni.

“Kitambo walanguzi walikuwa wanatoka ughaibuni lakini sasa hapa Pwani walanguzi wamekuwa wengine sana na wanafanya hiyo biashara haramu,” akaongeza .

Hata hivyo pia biashara hiyo maranyingi imehusishwa watu wanaoishi na ulema kutumiwa na kuekwa katika meneo ya katikati ya jiji la Mombasa na kuomba msaada. Hamisi anasema alijaribu kutembelea ubalozi wa kenya nchini Saudi lakini ubalozi huo haukumsaidi na hata ukamwambia afadhali aendelee kufanya kazi pasipo kumsiliza kilio chake.

Anaushukuru ubalozi wa taifa la India ambao ulimsaidia katika kufanya juhudi za kurudiha humu nchini ambao alirudi kwa kutumia ndege inayotumika kubeba wakimbizi.

“Mimi ninavyosema ubalozi Kenya katika mataifa ya nje hausaidii kabisa ,niwapelekea malalamishi yangu lakini sikupata msaada wowote.Ninaushurua ubalozi wa India ambao ndio ulinisaidia nikaweza kujinusuru kutoka Saudia,”akasema Hamisi.

Hamis anasema mawakala wengi wanaituma fursa hiyo kuwalaghai watu na kuwaacha watu katika mikononi mwa watu ambao wanawatesa watu katika mafia ya Ughaibuni .

Mwenyekiti katika kamati inasimamia ulanguzi wa binadamu humu nchini Goerge Masese amesema hali hioyo imechangiwa na kupungua kwa makali sheria inadibithi biashara ya ulanguzi wa biashara ya binadamu.

Masese amesema mara nyingi biashara hiyo inafanya na viongozi wa tabaka za juu huku akisema hivi karibuni kamati hoiyo itahakikishakuwa sheria kali zinachukuliwa kwa wahusika ambao wanafanya biashara ya ulanguzi wa binadamu.

Mataifa ya Afrika ya kati ,Bara Ashia na Uropa yangali masoko makuu ya wahanga wa ulanguzi wa binadamu kutoka eneo la pwani ambao hung’olewa viungo vya mwili na kuuzwa.