Countdown: Mwaka huu mpya tusisahau kujijali kwanza

Loading Article...

For the best experience, please enable JavaScript in your browser settings.

Mwaka mpya wapiga hodi. Mwaka ambao wengi wana matajario ya mema na bora kutokea.Japokuwa huo ndio mtindo, makala haya yataangazia baadhi ya mambo ambayo hatufai kamwe kutarajia mwaka huu.

Naam, ni vyema kuwa na matarajio mwaka unapoanza kwa kuwa huwa inaongeza ari na hamaki ya kutia bidii lakini ni vyema kujua kwamba baadhi ya mambo hayataleta ufanisi maishani mwetu. Kwa kabisa tutambue kwamba kwenda kanisani na kusema kwamba baraka zako umezipokea kwa kuwa mchungaji amesema haitoshi.

Ni kawaida ya waumini wengi kupenda kwenda kesha usiku wa kuvuka mwaka lakini tutambue kwamba hata tunapovuka mwaka na kupiga vifijo na vigelegele ni vyema kujua kuna mambo hayatokei hivi hivi.

Vifijo na vigelele vinavyopigwa kanisani havifai kamwe kukuhadaa kwamba baadaye kukipambazuka mambo yote yatakuwa sawa bila bidii yako. Vifijo hivi huwa vya kuashiria furaha kwamba tumevuka kutoka mwaka mmoja hadi mwingine salama. Unafaa utambue kwamba kila kitu unachokitaka mwakani kinafaa kutokana na bidii; na matarijio uliyo nayo yatatimia tu endapo utaelewa kwamba mambo yote yanakutegemea wewe.

Si hilo tu, bali ni vyema kutambua kwamba maishani kuna mengi ya kutekelezwa kando na kupiga kelele. Pili, mwaka huu tunafaa kutambua kwamba hatufai hata kamwe kupiga domo ovyo ovyo.

Mwaka huu tunafaa kujua kwamba ili tupewe heshima mijini na vijijni ni bidii yetu itakayo tuongoza. Hebu tafakari kuhusu yule tajiri umjuaye aliye kijijini na mwingine aliyejijini. Atajulikana kwa sababy gani? Kupanga kazi na kutimiza au kupiga domo?

Domo kaya hakuna siku litakufaidi na nwishowe litakuletea maafa. Ni shida tupu tusipotambua ukweli huu. Ubora wa maisha si kuruka ruka na kutapatapa kwa mambo yasiyokufaa bali ni kutambua kwamba una jukumu la kutekeleza na jukumu hili ni kuondoa kila tatizo lililombele yako.

Hoja ya tatu ambayo lazima tuache mwaka huu ni tabia ya kutegemea watu. Nani aliyekuambia kwamba wapo baadhi ya watu wasiokuwa na matatizo?

Nani aliyekuambia kwamba wapo watu waliona pesa tele za kukupa wewe? Hakuna aliyena muda wa kusumbuana na wewe. Watu wanahoja na shida zao. Wanasumbuliwa na matatizo yao.

Wanafikiria kuhusu jinsi watavyowekeza na kujenga majumba mazuri ya kuishi na familia zao. Si wewe…

Hivyo basi, tunapoelekea mwaka mpya, tuwe makini kuhakikisha kwamba tunafurahia na kutilia maanani maneno la sivyo tutakuwa na mwaka wa watu waliona majonzi ya kujitia.

Hata waswahili walikesha sema kwamba mwiba wa kujidunga hauna kilio. Wanatafakari nawataki mwaka mpya wa 2022 usiokuwa na mushkil wala kusumbuana. Tuwe na mwaka wa amani na kujijali.

Facebook: Stephen N Mburu

Twitter: MwandishiMburu