IEBC yasema Malala alipanga afisa wake adhalilishwe, Matungu

Na Carren Omae

NAIROBI, KENYA: Tume ya Uchaguzi IEBC imemtaja Seneta wa Kakamega Cleophas Malala kuwa aliyepanga kudhalilishwa kwa afisa wake wa Kike kwenye eneo la Matungu siku ya Alhamisi, wakati wa Chaguzi ndogo.

IEBC imemtaja Malala kweney taarifa yake leo hii huku ikishtumu ghasia zilizotokea wakati wa shughuli hizo zilizofanyika kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Kulingana na tume hiyo kundi la vijana lililopangwa na Malala, kulimdhalilisha na kumkosea heshima afisa wake kisha kumwondoa kwenye kituo kimoja cha kupigia kura.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema wanaapanga kuwaoa ushauri nasaha maafisa wake waliodhulumiwa, akisema tume hiyo imejipanga kuhakikisha chaguzi zinazofanyika nchini ni za huru na haki.

IEBC ilifanya chaguzi ndogo za Maeneo Bunge ya Mataungu na Kabuchai kwenye kaunti ya Bungoma huku chaguzi ndogo zikifanyika katika wadi ya Kiamokama kwenye Kaunti ya Kisii, Kithure/Kitise katika Kaunti ya Makueni, Huruma kwenye Kuanti ya Uasin Gishu, London na hell's Gate katika Kaunti ya Nakuru.

IEBC imeelezea wasiwasi kufuatia ghasia zilizoshuhudiwa ikisema zinatishia uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani. Imethibitisha kwamba hakukuwapo na visa vyovyote vya ghasia kwenye wadi za
Huruma na Kistise/Kithuke .

Related Topics

Malala Afisa