Alazwa katika Hopitali ya Kericho kwa shukiwa kuwa na dalili za Ebola

Mwanamke anayeshukiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa ebola alazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kericho.

Wahudumu wa afya katika hospitali hiyo wamesema mwanamke huyo alikuwa amesafiri kutoka Malaba alikoenda kumtembelea mpenziwe kabla ya kuanza kuonesha dalili za ugonjwa huo. Kwa sasa amelazwa katika chumba kilichotengwa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo iwapo anaugua.

Taarifa hii inajiri wakati Serikali ya Kenya ikiendeleza juhudi za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo hadi nchini Kenya kufuatia kuripotiwa kwa vifo viwili katika taifa jirani la Uganda. Kwa sasa wasafiri wote katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege, JKIA hasa wanaotoka mataifa yaliyoathirika wanakaguliwa kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini.

Kadhalika, vyumba maalum vitengewa na madaktari kuwekwa katika hali ya tahadhari iwapo atapatikana msafiri mwenye dalili za ebola. Katika mpka wa Busia kila anayeingia nchini anakaguliwa huku maafisa wote wakipewa mavazi maalum ya kuzuia maambukizi wakati wa kuwakagua wasafiri.

Miongoni mwa dalili za ebola ni joto jingi, maumivu ya kichwa na misuli, kutapika na kuendesha. Hata hivyo, dalili kuu ni kutokwa damu katika sehemu mbalimbali za mwili japo ili kuwa na hakika lazima kutafuta ukaguzi na ushauri wa daktari.

Related Topics

Ebola