Kesi dhidi ya Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu katika Mahakama ya Milimani imesitishwa kuambatana na agizo la Mahakama Kuu. Hakimu Lawrence Mugambi ametoa uamuzi huo baada ya kupokezwa maagizo sahihi kutoka kwa Jaji Chacha Mwita wa Mahakama Kuu baada ya kurekebisha dosari zilizokuwapo katika agizo la kwanza.
Hakimu Mugambi hata hivyo amesema kikao kingine kitaandaliwa Oktoba 22 wakati mahakama itakapofahamishwa kuhusu yaliyoafikiwa katika Mahakama Kuu ambapo Jaji Mwilu amewasilisha kesi kupinga kushtakiwa kwake katika mahakama ya hadhi ya chini vilevile kuishtaki ofisi ya DPP na ile ya DCI kwa misingi ya kulenga kumdhalilisha.