Kiwanda cha kutengeneza vileo cha Keroche kinatarajiwa kufunguliwa leo hii. Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi KRA itaongoza hafla ya kukifungua kianda hicho mjini Nakuru.
Hatua hii inafuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu iliyoiagiza KRA kukifungua kiwanda hicho hadi kesi iliyowasilishwa na Afisa Mkuu Mtendaji Tabitha Karanja itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Karanja aliwasilisha kesi mahakamani dhidi ya KRA kwa kupuuza agizo lililotolewa awali kuiruhusu keroche kuendelea na biashara.
Kiwanda hicho kilifunga tarehe 22 mwezi Mei kwa kushindwa kulipa kodi ya shilingi milioni 957 inayodaiwa na KRA.
READ MORE
How 300 containers were stolen from Mombasa port
Mbadi names Adan Mohamed as new KRA chief
Mass Ukraine drone barrage kills 3 in Russia: Moscow
Ex-CS Adan Mohamed front runner for KRA top job despite age limit hitch