Sultan Qaboos bin Said wa ufalme wa Oman na binamu wa Sultan wa Zanzibar.

Mmoja wa familia ya Sultan wa Zanzibar na ambaye amekuwa mfalme wa miaka mingi katika himaya za kiarabu, Sultan Qaboos bin Said, binamu wa Sultan wa mwisho wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah al Said ameaga dunia nchini Oman.

Kifo cha Sultan Qaboos kwa Wakenya chungu nzima hususan katika mwambao wa pwani ya Kwale, Mombasa, Kilifi, Malindi na Lamu ni afueni kutokana na mwamko mpya ambao mwendazake alikuwa ameanza kusukuma vizazi wa Sultan kurudi kunyang’anya ardhi wapwani ambao wamekalia ardhi ambazo Warabu wa Oman walinyakuwa awali.

Sultan Qaboos bin Said aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 79, Jumamosi ya Januari 4 mwaka huu baada ya kuongoza ufalme wa Oman tangu mwaka 1970 alipopindua serikali ama uongozi wa baba yake mzazi kwa usaidizi wa Uingereza akiwa na umri wa miaka 29.

Miaka ya hivi karibuni, Sultan Qaboos amekuwa akitumia turathi za ukoloni wa Sultan wa Zanzibar na Oman (binamu) yake ambaye alifurushwa mwaka 1964 na mamluki wa asilia ya Uganda, Brigedia John Gideon Okello.

Qaboos amekuwa akishirikiana na viongozi wa maeneo yenye turathi kukagua raslimali ambazo zimeachwa na vizazi wa Sultan pwani ya Kenya kuchochea kupitia wanasiasa wanaoshirikiana kimaadili na wawakilishi wake kuteka raslimali hizo.

Binamu yake na Sultan wa mwisho wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah ambaye yungali makao yake alikokimbilia ya Postmouth nchini Uingereza vile vile amekuwa akiwatumia washirika wake pia kunyemelea ardhi ambayo kulingana na wakongwe wa masuala ya kikoloni, alilipwa kikamilifu ridhia zake na Uingereza na serikali ya Kenya.

Jamshid ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 90, anaishi maisha yake ya unyekevu nchini Uingereza tangu kubanduliwa Zanzibar mnamo mwaka 1964 na wananchi wa Zanzibar yasemekana kwa pamoja, walimsamehe madhambi yake yote kwenye ujumbe walioutoa mwaka 2010.

Ujio wa Sultan Mababu wa Sultan Jamshid Abdullah na Sultan Qaboos bin Said wakiongozwa na Seyyid Said na Seyyid Barghash ndio wa mwanzo kuwasili afrika mashariki ya Zanzibar kama wafanya biashara.

Huu ulikuwa mwaka 1832 na kuamua kwa tamaa yao kuufanya mji huu makao makuu badala ya kwao Muscat.

Bila hata kushauriana na wapwani wa maeneo husika, Wanyama hawa walijumuisha miji inayokurubana na bahari hindi kuanzia Bahrain, Cabo Delgado, Pemba, Lamu, Malindi na Mombasa kuwa yao, unyakuzi wa kulaaniwa milele.

Ni hawa wakoloni wa Oman ambao walitumia wenyeji kama watumwa kuwalimia mazao ya biashara na chakula kwenye mashamba yao makubwa na yakumbukwa kwamba ni huyu Seyyid Said aliyepanga kumuua mjomba wake kwa jina la Badr ili achukue nafasi yake kama Sultan.

Akiwa na umri wa miaka 16, Seyyid Said aliagiza muaji wa mjomba yake amchome kisu moyoni. Wakati Warabu wa Oman walipofi ka pwani, waliwakuta maliwali wa Mazrui ambao walikuwa wamemita mizizi hususan Mombasa.

Sultan bin Ahmad wa Oman (Muscat) alipochukua hatamu miaka ya 1790s, dhamira yake ilikuwa ni kutawanya uongozi wake kufuatia ugomvi ndani ya ufalme wake.

Kufi kia miaka ya 1850s, bado wakiwa wakishirikiana na mabepari wa Uingereza, walijigawa ufalme wa Oman, mmoja ule wa kina Jamshid bin Abdullah ambaye alitolewa 1964 kama Sultan wa mwisho wa Zanzibar na mwingine ule wa marehemu Sultan Qaboos bin Said aliyeaga dunia hivi punde akiwa Sultan wa Oman.

Mapinduzi ya Zanzibar 1964 Wadadisi wengi leo wanazungumzia mapinduzi ya kuwatimua Wa-Oman wa Zanzibar mwaka 1964 yaliyoongozwa na mamluki wa kiraia wa Uganda, John Gideon Okello kuwa tiba ya milele ya tatizo ya ardhi nchini humo ukilionganisha na sehemu za pwani ya Kenya.

John Okello ambaye alikuwa akitafutwa nchini Kenya kwa tuhuma ya kunajisi hadi kuwahi kukamatwa, hatimaye aliamua kujitoa mhanga kuwa mkombozi wa wenyeji na ndugu waafrika wenzake wa Zanzibar kwa kuongoza mapinduzi ya kuwafurusha Wa-Oman na vizazi ambao baadaye walirotokea Mombasa kutua kwenye ardhi zaidi kuendeleza ukandamizaji wao.

Ni huyu John Okello ambaye alifaulu kumalizana kabisa na utawala wa Warabu halisi wa Oman katika Zanzibar.

Jitihada zake za kutotaka dhulma kwa wanyonge hatimaye ziliwapa motisha wengine hadi kuripotiwa vute ni kuvute ya kijeshi nchini Kenya, mwezi mmoja na nusu baada ya Uhuru ambapo wanajeshi katika kambi za Lanet na Lang’ata walizusha rabsha kiasi juu ya mishahara. Hali iliripotiwa vivyo hivyo katika mataifa jirani ya Uganda na Tanganyika wakati huo mmoja.

Maafa ya 1964 Licha ya kiongozi wa mapinduzi hayo ya Zanzibar, John Okello kuwahimiza wanajeshi wake ama wanamgambo (mamluki) kujiepusha na unyama wa kunajisi na kudhuru watu wakati wa fagia-fagia yao, kumbukumbu ya taarifa zake, zahuzunisha mno kwani visa vya bikra kubakwa, mauaji ya kinyama na kadhalika vimethibitishwa.

Ripoti zasema kuwa maelfu ya wanawake walibakwa na watu wengi kupoteza maisha yao. Maafa ya ghasia hizi za mapinduzi zaonyesha zaidi ya watu 20,000 walipoteza maisha yao. Ingawa hivyo, John Okello alisaidia kumaliza utawala wa Wa-Oman nchini Zanzibar.

Kulingana na bahari ambazo hazijaaminika vyema kutoka kwa maktaba ya kihistoria ya mkombozi Okello, yaaminika John Okello aliuliwa na rafi ki yake mwenyewe, Id Amin Dada mnamo mwaka 1971.