Leo hii kama kweli baraza la wazee wa jamii ya Wakamba wangelitambua dosari lililosababishwa na gavana wa Machakos, Alfred Mutua kwa wanaume chungu nzima wa Kenya na barani Afrika, yamkini wangeitisha kikao cha dharura kumpa kisomo gavana huyu.
Kisomo cha kwanza ni kumuonya wazi kwamba ni mtoto peke yake ambaye anaweza kulalamika kunyanyaswa na mtoto mwenzake lakini siyo jibaba lenye cheo cha ugavana kama yeye, kulalamikia juu ya mwanaume ama wanaume wenzake.
Kazi rahisi angejitokeza kwa kuitisha mkutano mkubwa katika kaunti yake na kuwapasha wanaomtishia kwamba dawa ya moto ni moto lakini siyo maji.
Katika mila nyingi za Afrika, mwanaume huogopa kumpoteza mkewe kwa mwanaume mwenzake lakini siyo kutishiwa maisha yake na ndume kama yeye.
Hii ina maanisha kwa kilio cha mtu mzima Gavana Alfred Mutua wa Machakos kuwa wanaume wenzake Naibu rais William Ruto, mbunge Aden Duale na seneta Kipchumba Murkomen wamtishia maisha ni aibu kwa wanaume wote na wakamba kwa jumla.
READ MORE
YouTuber claims he was threatened by Sudi for criticizing Ruto
Ruto shifts focus to Western and gives restless Mt Kenya wide berth
Mumias Sugar farmers set to receive bonus payout
Sugarcane farmers welcome Ruto's promise to pay bonus in January
Mwanaume kamili anaogopa kuabika kutofanya majukumu yake ya kifamilia lakini siyo kifo wala ngumi. Wengi wanaamini kuwa mtu alizaliwa siku moja na atakufa siku moja.
Kilio cha mtu mzima Waswahili wanasema kuwa ukimuona mzee mzima anabubujikwa kutoa machozi, ujue kuna jambo. Mapema wiki hii, Gavana wa Machakos alijitoa hadharani kudai kwamba anatishiwa maisha yake na Naib rais Ruto, mbunge Duale na seneta Murkomen ambao wanasemekana walimtupia cheche za maneno makali ambayo kisiasa ni lazima.
Isitoshe, aliandikisha taarifa kwa polisi na kuisema hadharani kwamba wakati kwake umefi ka kuweka wazi vitisho vinavyomkabili ijapo hakufafanua zaidi isipokuwa hisia kwamba matamshi yao pengine yamemlenga kwa njia moja au nyingine.
Sasa basi, wadadisi ambao walikuwa na maoni mbali kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na lalama ya gavana Mutua, wanaongezea shari vitisho vyake kwamba mbali na kutishiwa maisha yake, huenda pia ndoa yake inatishiwa na ndume anazozungumzia kwa wepesi wao wa kunyakua majiko sawa na lake.
“Endapo kutatokea tukio lolote baya au lisilo la kawaida kwenye familia ama jamii yangu, hawa watatu Ruto, Duale na Murkomen watakiwa kuchunguzwa”, Mutua alizungumzia vyombo vya habari punde tu baada ya kuandikisha taarifa yake katika kituo cha polisi cha Kilimani jijini Nairobi.
“Hali kadhalika nimeagiza kuongezewa walinzi zaidi wa kibinafsi kwa kuhofi a maisha yangu,” anaongeza Mutua.
Afisa Mkuu wa Upelelezi katika Kituo cha Polisi cha Milimani Fatuma Hadi alisema polisi wameanzisha upelelezi kuchunguza madai hayo.
Uhasama kati ya Naibu Rais na Gavana Alfred Mutua unatokana na hatua ya Mutua kupuuzilia mbali mapendekezo ya aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama anayeaminika kuwa mthamini mkuu wa Chama cha Wiper kwamba Ruto abuni muungano na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Tangu Kenya ijinyakulie Uhuru, wapinzani wakuu wa kisiasa wamepoteza maisha yao kwa njia ya kutatanisha wakiwemo Pio Gama Pinto, Tom Mboya, Ronald Ngala, J.M Kariuki, Robert Ouko, George Saitoti na wengineo.
Wakati wa utawala wa mwanzilishi wa Taifa Mzee Jomo Kenyatta na Rais Mustaafu Daniel Arap Moi kulikuweko na mawaziri waliokuwa na ushawishi mkubwa waliowazingira viongozi hao na hakuna mtu angeweza kuleta nyokonyoko au akione cha mtema kuni.
Kila uongozi haukosi wadhamini ambao wana sauti na wanahudumu kama walinzi wa wakuu wao hivyo basi kucheza na watu kama hao ni sawa na kucheza na viongozi wenyewe kama ilivyodhihirika kwenye taarifa ya Alfred Mutua kwamba Adan Duale na Kipchumba Murkomen ni wandani wa karibu wa Naibu Rais Dr. William Ruto na kwamba hatua zao zinawakilisha hatua za Bwana Mkuu wao.
Mwanaume kamili Kwa mwanaume kamili, Mutua hangesubiri kuonyeshwa madharau ndani ya ikulu bali angekuwa ngangari kinoma ya kuhakikisha kwamba yeye pia ni mkuu wa kaunti ya Machakos na wala hakuna mbuzi kuruka mbele yake.
Katika kisa chake cha kwanza mnamo Novemba 25 mwaka huu, anasimulia kwamba alitishiwa ndani ya Ikulu ya rais na Aden Duale na Kipchumba Murkomen siku ya upokezi wa ripoti ya BBI.
Ni hapa ambapo anasimulia kinaga ubaga kwamba ushari wao kama ifuatavyo;
Duale: Wewe gavana nini mbaya?
Mutua: Waamanisha nini?
Duale: Umekuwa ukituingilia sana sasa utatutambia.
Mutua: Nimewaingilia kivipi?
Murkomen hapa anaingilia: Wewe wacha zako lazima tukupe funzo.
Mutua: Nimefanya nini jameni? Lini niliwahi kuwaingilia kati yenu nyinyi?
Duale: Ukiingilia kundi letu, sawa na kuingilia sisi!
Mutua: Kundi?
Murkomen: Umekuwa ukimwingilia kisiasa naibu wa rais.
Duale: Ukimgusa DP unatugusa sisi!
Mutua: Mbona siwaelewi wangwana.
Mheshimiwa Duale si wajua tumetoka mbali na wewe vizuri.
Murkomen: Huyu niachieni mimi nimpe funzo.
Ni wakati huu ambapo ambapo Gavana Mutua angewachemkia kama mwanaume kwa kuwazima vitisho vyao hata kama ni kwa kuzua sarakasi ili viongozi wengine wagutukie kwamba kunalo vurumai.
Hivyo, kilio chake kingeanza kushughulikiwa mapema.
Lakini la kustaajabisha ni kuwa kulingana na taarifa yake, aliendelea kuwabembeleza Duale na Murkomen hivyo kuwapatia pembe za kumfokea ilhali ni mwanaume mwenzao na labda kiongozi wa wadhifa mkubwa kuwaliko.
Labda, wakati Gavana Mutua alipokuwa hajabanduka kwa muungano wa kambi ya naibu rais William Ruto na kurejea kwa kinara wa upinzani Raila Odinga, huenda akawa aliwahi kulamba asali ambayo Duale na Murkomen waliowahi kushuhudia nyakati zao za urafi ki wa Mutua na Ruto, wanataraji kulipiza deni lao.
Katika kuchambua majibizano yao, utaona ya kuwa Mutua alikuwa na unyenyekevu mwingi na kutaka kuwabembeleza Duale na Murkomen jambo ambalo lawatia wengi kiwewe ni kwa nini alikuwa na unyonge huo badala ya kuwakemea kama kiongozi.
Ruto, Duale na Murkomen hakuna kura yake ambayo ilimuongezea ushindi wake Machakos hivyo mbona awachekelee wakimkaranga kama njugu?
Awamu nyingine ya taarifa yake ni pale anapozungumzia ukaidi wa naibu rais wakati walipokutana siku ya ziara ya kiongozi wa taifa la Barbados, Waziri Mkuu Mia Motley alipotembelea Ikulu ya Rais mnamo Desemba 11, 2019.
Mutua hali kadhalika hapa anadhihirisha unyonge wake kinyume na mwanaume kamili wa kiafrika kwa kukimbilia kinara wa upinzani Raila Odinga kulalamika kwamba amefi nywa mkono na kuongeleshwa visivyo na naib rais William Ruto.
Mutua: Jambo Mheshimiwa Naibu Rais wa jamhuri ya Kenya?
Ruto: (Akiwa amemmbana mkono wake wa kulia) Wewe jamaa umekuwa ukinichapa sana kisiasa! Mutua: Mheshimiwa naibu rais! (Huku mkono ukiwa bado umeshikwa vilivyo).
Ruto: Wewe lazima sasa nikugonge. Nitakugonga. Mutua: Mheshimiwa naibu rais, labda tunaweza kuzungumzia suala hilo….
Ruto: (akimsogesha Mutua kutoa njia anayopita) Wewe ngoja utaona.
Duale: (akimuotea Mutua kidole) Si tulikuambia…
Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanachambua majibizano haya kama mchezo wa kisiasa na wala gavana Alfred Mutua hakuwajibika kujitetea papo hapo. Wengi wanasema kuwa fikra zake kwamba atagongwa, hajui ni kugongwa kisiasa majukwaani ama kuwekwa kwenye parawanja kuhusiana na jinsi walivyokuwa marafi ki mbeleni.