Kama kunalo fungu la watu ambao wamechezwa shere miaka mingi katika mipangilio ya mfumo unaoletwa na mapendekezo ya BBI, bila shaka ni Wakenya wanaoishi jimbo zima la pwani ya Kenya. Wameshuhudia BBI chungu nzima tangu jadi ya kuwakaribisha wageni wa mwanzo ambao hatimaye waliwageukia kuwafanya bidhaa za kuwauzia milki za kigeni, Ghuba la uajemi na Bara Ulaya.
Fadhila ya kuwakaribisha wageni hawa ilikuwa ni utumwa wa kuuzwa wakiwa wamefungwa nyoyoro miguuni. Kuona BBI yao ya kwanza Pwani ilikuwa mwaka 1895 walipopigwa mazingaombwe na Mwarabu na Mzungu kuhusiana na raslimali na mali ya mwambao wa pwani wakipuuzwa baadaye na usimamizi wa himaya za Sultan wa Oman na Zanzibari.
BBI yao ya pili ikawajia mnamo mwaka 1908 wakati Mwingereza alipanga njama na Mwarabu na Malkia wa Uingereza kunyakua ardhi za wenyeji kwa madai kwamba wanatafutia mikopo ya wakulima wazungu, warabu wa Sultan kwa minajili ya kutoa mazao ya kusa? risha hadi Ulaya.
Ni nyakati hizi ambapo mvua ya dhuluma ya ardhi kwa mpwani halisi ilianza kumchapa kwa kumnyeshea mfululizo wa miaka nenda, miaka rudi. BBI ya tatu ni pale vita vya ulimwengu (vita vya kwanza vya dunia) 1914 vilipoanza na Wazungu wakoloni walipowarai kwa lazima mababu zetu kushirikishwa kwenda kupigana vita ambavyo hawakujua chanzo chake wale sababu ya kupoteza maisha yao. Hali ilikuwa hivyo hivyo mnamo katika vita vya pili vya dunia miaka ya 1940s.
READ MORE
First-term curse: Why every new president faces a crisis right after being sworn-in
National Treasury explores PPP models for mega projects after Adani Group exit
BBI ya Ngala na Jomo
Huku tukiwa tumeanza kuisoma ripoti iliyozinduliwa juzi ya BBI, wapwani wengi wangali wakitingisha vichwa vyao kutafuta sentensi ama kifungu ambacho kimegusia marekebisho fulani ambayo yanaweza kuwapa matumaini ya kuwatoa kutoka janga la hujuma za kihistoria. Wao walidhani kuwa baada ya katiba ya 2010 kukosa kifungu cha aina hiyo na ripoti ya TJRC kusumbikwa mvunguni, waliona kheri safari hii ripoti hii itagusia. Hali hii inazusha kumbukumbu yam waka 1964 ambapo viongozi Ronald Gideon Ngala na Jomo Kenyatta walikuja na BBI yao kwamba Ngala ashirikishe KADU na KANU ili waendeleze katiba moja ya majimbo ambayo ilitoa nafasi ya uhuru wa Kenya. Hatimaye, makubaliano haya yalipigwa teke wakati KANU ilishinda uchaguzi na katiba ya majimbo ikatupiliwa mbali.
Suala hili latupa mfano gani?
Hii inamaanisha kwamba “hendisheki’ haijaanza leo baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga. Taifa la Kenya linayo historia ndefu ya siasa za aina hizi tangu mwaka 1962. Ile “handisheki” ya kwanza ilikuwa baina ya chama cha KADU na Waingereza waliokuwa wamezagaa humu nchini. Wakati walipojua kwamba ni dhahiri Kenya itakuwa huru karibuni, Wazungu waliegemea mrengo wa KADU ambao uliwakilisha makabila madogo ambayo yalikuwa yemetiwa ubimbi na muungano wa makabila makubwa ya Wakikuyu na Waluo waliokuwa chini ya KANU. Ripoti za ndani zaeleza kuwa sababu ya Wazungu kuhusudu KADU ni kwamba hawakuamini mfumo wa KANU kwa kimombo “The Nationalist Movement” kwamba radhi yao na haki zao zitakuwa hatarini iwapo serikali itaangukia uongozi wake. Hali ilifanya “hendisheki” ya wazungu na KADU kuwa maarufu na tisho kwa wapinzani wa Ronald Ngala. “Hendisheki” nyingine maarufu ilikuwa baina ya Ngala na Jomo Kenyatta alipohusika kama mkinara wa serikali wa kwanza ya upokezi wa mamlaka baina ya Uingereza na Kenya na kuhusika kushawishi kuachiliwa kwa Jomo Kenyatta kutoka gerezani. Inakumbukwa kwamba “hendisheki” yao ilishuhudia punde tu KANU iliposhinda uchaguzi mkuu wa 1963 ambapo Jomo Kenyatta alikubaliana na Ngala waendeleze katiba ya majimbo kwa kimombo “Federal Constitution”
ambayo ilikuwa kati ya vikwazo vya mwingereza kabla ya kupoeana uhuru kamili kwa taifa la Kenya. Ni wakati huu ambapo pia tofauti zilizuka baina ya mrengo wa Kenyatta na Ngala jinsi ya mfumo wa serikali huku Ngala akishindwa na mpango kuthibiti majimbo hivyo mfumo wa chama kimoja ukazinduliwa tofauti kabisa na vile mwandani wake Jomo, Jaramogi Oginga Odinga alivyokusudia. Mfumo mwingine sawa na huu ulijitokeza mnamo mwaka 1997 baina ya chama cha KANU na upinzani walipokuja pamoja kukabiliana na mchipuko wa mashirika ya kijamii na janga la maandamano ya kupinga uchaguzi mkuu uliokuwa unakaribia. Ni “hendisheki” hii ya 1997 ambayo ilizaa babake BBI almaarufu IPPG (Inter Parties Parliamentary Group). Mnamo mwaka 2002, muungano mwingine wa NAK ulizaliwa kutoka kwa mwingine wa NAC kabla ya huo huo kufunga ndoa tena na mwingine kupitia chama cha LDP na kuzaa muungano mashuhuri ulioshinda uchaguzi mkuu wa 2002 wa NARC.
BBI ya Kibaki na Raila
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2017, mnamo 2008, miaka kumi kabla ya Uhuru na Raila kuwa na fungate yao 2018, Rais Mwai Kibaki wakati huo na kinara wa upinzani Raila Odinga walishikana mikono “hendisheki” kama njia muafaka wa kumaliza ghasia za uchaguzi (2007-2008) kufuatia mazungumzo ya miezi miwili ya amani chini ya uongozi wake mwendazake Ko? Annan. Maridhiano yao Kibaki na Raila, yaliweza kutuliza nchi na kuleta amani kwa kuzindulia serikali ya nusu mkate kwa kimombo “Grand Coalition Government) hali ambayo ililazimu kufanyike marekebisho ? nyu ya kikatiba kuweza kuwepo kwa nafasi zaidi za uongozi. Kukazaliwa nafasi ya Waziri Mkuu na manaibu wake zaidi ya rais na makamu wake. Shabaha na lengo la BBI ya leo bila shaka yalenga papo hapo lakini dhuluma ya kihistoria kwa wanyonge imewekwa wapi?