Huku maafi sa wa idara za EACC na DCI zikiwazamia mameneja wakuu wa halmashauri ya bandari nchini, KPA, mengi yazidi kujitokeza kwamba huu ni mtego wa abunuwasi utakaowanasa waliomo na hata wale wasiokuwemo.
Bandari hii ya KPA, imegeuzwa kuwa uwanja wa fujo, karaha, unyanyasaji, utapeli, kisiwa cha giningi na kitega uchumi kwa wanasiasa wakubwa wanaosimamia makundi yote mawili ya “Handisheki” na “Tanga Tanga”.
Nyani haoni dudele
Leo hii licha ya mameneja wakuu wa KPA wakiongozwa na MD Daniel Manduku na Capt. William Ruto kuwa chuma chao kimo motoni, baadhi ya wanasiasa mashuhuri nao hawapati usingizi wa kutosha tangu Rais Uhuru Kenyatta kubweka juzi kuwa aliomiza fudu (kuiba pesa) za umma bandarini, wajipange watakavyo zinya.
Wasi wasi ni kuwa mmoja wa kinara wa “Handisheki” na BBI asemekana kutumia ushawishi wake mkubwa wa kisiasa kumzawadi mtoto wake zabuni za shilingi milioni 460 kutoka KPA kati ya mwezi Januari na Julai mwaka huu.
READ MORE
Put Kenyans first, not critics- Gachagua blasts Ruto
Karua to Ruto: Manage your anger and stop insulting Kenyans
President Ruto blames political unrest for delayed county funds
Naye mwingine kigogo cha “Tanga Tanga” na mrai wa msukumo wa “Punguza Mzigo” yaaminika yungali akitumia misuli yake ya ushawishi bandarini kuvuna mamilioni ya pesa kupitia maneja fulani walio marafi ki wa kufa na kuzikana.
Ni mwanasiasa huyu ambaye anasemekana kwamba alihusika mno na msururu wa kuleta mahindi nchini kupitia mlango wa nyuma wa KPA akimtumia mtoto wake kuja kukagua shehena nyakati za usiki mbele ya mameneja wakuu bandarini.
Hata kabla ya Rais Uhuru Kenyatta kuja kuwafokea wasimamizi wakuu wa bandari hivi punde, tayari vita baridi baina ya mameneja, wanasiasa mashuhuri na maafi - sa wakuu serikalini walikuwa wameanza kutemeana mate (kukashifi ana wenyewe kwa wenyewe) juu ya kurushana mamilioni ya pesa katika zabuni mbili za kimataifa.
Paka na Panya
Chanzo cha mameneja wakuu wawili Dkt Daniel Manduku (Mkurugenzi mkuu KPA) na mchini wake Cpt. William Ruto kuanza kuvutana ni upwagu na upwaguzi wao kuhusiana na zabuni mbili (kandarasi) za kununua mashua mbili maalum za TUG BOAT na SALVAGE BOAT.
Salvage Boat (Mashua ya uokozi/usaidizi): Zabuni hii imegawanya mameneja wakuu wa bandari kutokana kwamba mfunga ngozi daima huvutia kwake. Hii ni zabuni ya kimataifa na kandarasi yake ya kunua inagharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.7.
Kampuni ambazo zilipigwa msasa na kukaguliwa kupita mkondo wa kwanza ni tisa huku kila meneja akimezea mate donge aidha kutoka kampuni fulani shiriki hivyo ikawa ni mume nguvuze. Kampuni zilizoshiriki ni kama zifuatazo; Grandweld Shipyard U.A.E ikiwakilishwa na Bw.
Abdulgani Pasta, Yexin Ocean Engineering Ltd ikiwakilishwa na Stephen Karisa, Atuon (SA) ikiwakilishwa kwenye ufunguzi na J.J Pasalal, Samwon H.I ikiongozwa na Sang Lee, Bogarici Denizalik, Med Marine ikiwakilishwa na Tito Mutai, Cheoy Lee Shipyards ikisimamiwa kwenye ufunguzi na Steve Munga na ile kampuni ya Tor Marine ambayo iliwakilishwa na Alphonse Mbaru.
Mbarika yavunjika
KPA Wengi yasemekana walianza kununa wakati ilipofi kia zamu ya kamati ya ukaguzi wa zabuni kwa kampuni zilizofuzu kuchungwa zaidi. Kamati hii yaaminika inaongozwa na mwenyekiti ambaye yumo mfukoni kwa maneja mkubwa wa KPA ambaye anasumbuana na mwenzake kuhusiana ni kampuni gani yastahili kupewa zabuni hii.
MD ambaye yaonekana kupata msukumo wa kasi kutoka kwa wakubwa wengine wa wizara, kadhalika aliamua kuwa ngangari kuhakikisha kampuni yenye uhusiano wa karibu na mtani wake wa KPA pia haijapewa nafasi licha ya kuwa awali ilitumia mbinu sawa kupata zabuni ya kunua TUG BOAT ya awali KPA.
Wandani wanazungumzia kampuni ya Cheoy Lee Shipyard kama inayotumiwa kunyemelea zabuni za kimataifa licha ya kuwa msingi na mandhari yake yajulikana kuwa chini ya watu fulani wanaowekwa kipao mbele na mwanachama wa vugu vugu maarufu la YK92.
Mameneja wamekuwa wakivurugana kwa ushindani wa kampuni mbili za Cheoy Lee Shipyard na ile ya Med Marine ambayo yadaiwa kusukumwa kutoka kwa wakubwa fulani wa Wizara ya uchukuzi yenye kumtumia meneja mwingine.
Katika mashindano yao, kila kampuni imejaribu kujibebea na bei huku moja ya Med Marine ikitoa yake ya mwisho ya Dola milioni 15.2 za Marekani nayo Cheoy Lee Shipyard ikitimia Dola Miioni 16.2 za Marekani kuweza kuleta mashua hizo.
Hadi kufi kia hapo, kila kitu kimekwamishwa na vurugu la mume nguvuze! Kwa kifupi wananyongana koo wawili kwa maslahi yao na wakubwa wao ilhali Rais Uhuru Kenyatta ambaye anajikakamua kukomesha ulaji hongo, yuaumwa na kuviviwa na watu wake mwenyewe.
Manduka adinda
Pilot Boat (Zabuni ya mashua ya nahodha) yenye kugharimu Dola milioni 6 za Marekani. Mkurugenzi mkuu Daniel Manduku twafahamishwa kwamba alichukua hatua ya kuisitisha zabuni hii ya PILOT BOAT baada ya kampuni ya Cheoy Lee kushinda zabuni ya kuijenga ama kuitengeza mashua hiyo kwa kitita hicho.
Hii inatokana kwamba utaratibu wa zabuni hiyo haukuwa wa haki na kufuatwa kisheria dai ambalo linaendelea kutajwa katika zabuni chungu nzima za bandari. Kizungumkuti kilibaini baada ya KPA kufanya ujanja wa kutuma ujumbe wa kamati ya ukaguzi wa zubuni hiyo kwenda Hong Kong kuchunguza kampuni endapo inao uwezo wa kutengeza mashua.
La kushangaza ni kuwa ni kampuni hiyo moja iliyoleta mashua nyingine juzi ya MV Eugene kwa bei ya Sh1.2 bilioni.
Uhuru kaza Kamba
Washikadau sasa wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta kukaza kambaa zake za kunyonga ufi sadi katika mashirika yote ya serikali ili kuchunga pesa za umma.
Madai ni kwamba siasa ya Tanga Tanga na Kieleweke na Handisheki zimevamia halmashauri ya bandari nchini kwa madhumuni ya kuteka pesa za kampeini ya 2022.