Wakenya wengi bado hawana ufahamu baina ya kundi la ‘Tanga Tanga’ na lile la ‘Kieleweke’ maana yao ni nini hasa. Kwa yule Mkenya ambaye hapendelei upande wowote wao, basi hubakia akijitazamia njonjera ama kwa lugha nyembamba ‘vitimbi’ vya watu wazima wenye wakwe na wajuu zao wakilumbana majukwaani.
Ngonjera zao hizi ambazo hazina tofauti na michezo ya kuigiza, zimefikia kiwango cha kuwatumbuiza jamii nchini
kiasi kwamba iwapo wanaelezea masuala muhimu ama yasiyokuwa na umuhimu bado hakuna mtu anaweza kuwathamini kwamba wanazungumzia mambo muhimu nay a busara. Mwana umleavyo ndivyo akuavyo.
Hivi karibuni, Wakenya wametumbuizwa na misemo ya mizaha ya wanasiasa na viongozi wengine ambao hutumia
READ MORE
Atwoli: Trump's presidency will restore Godly values
Fight to decriminalise attempted suicide gains momentum as cases surge
Atwoli criticises Gachagua for opposing Marikiti traders' relocation
Suspects linked to Oscar Sudi's club looting freed on police bond
ndimi (misemo) yao kama kivutio ama umaarufu. Wengine huwajibika kutamka maneno ovyo siyo kwa kuwa wamekosa nidhamu za kimsingi ya kijamii bali kudhihirishia wakubwa wao kisiasa kwamba wamejitoa mhanga siyo kisiasa tu bali hata mali na hali.
Lonyangapuo
Kijana mfupi wa raundi mengine ijapo ni ya kuwaudhi wengine wanaopashwa vijembe hivyo, kwa Wakenya huwa yanabakia ya vichekesho tu.
Kwa mfano, tuchukulie ule msemo uliotolewa hadharani na gavana wa West Pokot, Prof. John Krop Lonyang’apuo ya
“Kijana fupi (mfupi), amenona round (mnene) hujui tumbo lake liko wapi au mgongo uko wapi (mtu dungudungu)
ambao umechukuliwa kama kichekesho kote nchini.
Lonyang’apuo alitamka haya kwa hasira na mwishowe imeibukia kuwa nyota wa msemo huu ambao twaarifiwa
kila atakayemuona gavana huyu anakumbuka na kuangukia kicheko na kutaka kujua kwa ndani hasa alimaanisha nini wakati aimsuta kijana mfupi huyo. Huyu alikuwa anathibitishia wananchi wake wa West Pokot kiini cha naibu wake
kuwa nje ya nchi kwa muda mrefu mpaka wakereketwa kama kijana huyo mfupi akaanza kumkera.
Oscar Sudi
Huyu mbunge wa Kapseret amekuwa nguzo ya nyumba kisiasa katika kambi ya Naibu wa Rais William Ruto na amekuwa kwenye msitari wa mbele kulelecha maneno mazito yanayohitaji mizani ya kuyapima.
Yeye amenukuliwa mara kwa mara akijikuta akizungumza ama kutoa matamshi makali kukinga kinara wake endapo kumeezekwa lawama lolote lile. Hivi sasa anategemewa na kundi zima la kisiasa ya mpwito wa mkono wa kushoto la “Tanga Tanga’ kama kijembe cha kunyolea maneno yazukayo kutoka upande wa Bonde la Ufa ama Nyanza.
Ni hivi majuzi tu aliwajibika kwenda kujitetea katika tume ya uwiano wa kijamii baada ya kutoa matamshi
ambayo yangezusha chuki za kijamii. Lakini kwa kuwa waswahili walinena wakasema kwamba sikio la kufa huwa
halisikii dawa, Oscar Sudi haonekani kana kwamba amepunguza tabia hii kwani kila kukicha anaropokwa maneno yasiyokuwa ya kichwa wala miguu.
Atwoli vs Jumwa
Katika safu ya majabali haya mawili ya mdomo mfano wa kasuku, hivi sasa Wakenya wanatumbuizwa na msemo wa
hivi punde wa mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa ambaye bado anaonekana kukerwa kwa maneno ambayo katibu mkuu wa COTU, Francis Atwoli alitamka akiwa Lamu kwamba, kunao wagombeaji wengine ambao hawatafikia uchaguzini mkuu ujao wa 2022.
Kwanza, Aisha Jumwa alimjibu siku hiyo hiyo akiwa mkutanoni maeneo fulani ya Bonde la Ufa alikokuwa na mzururo wao wa kundi la ‘Tanga Tanga’ na kumfananisha na kijana wa Lonyang’apuo kwamba: “huyu anatuambia
nini ambaye hatujui tumbo lake liwapi na mgongo wake umewekwa wapi. Atwoli kama kawaida yake, tayari ameshapata tuzo kwa msemo wake “Sheenzi hawa” ambapo amewaorodheshwa wote wasioambatana na msimamo wake kamamazuzu.
Magari ya kifahatri
Wakati Atwoli alipomkejeli mwanasiasa mmoja wa jimbo la kati ya Kenya (Mwakilishi wa kina mama) baada ya kutofautiana kimsimamo wa kisiasa, mbunge wa Malindi Aisha Jumwa alirudi tena jukwaani naye akimkejeli katibu
kwamba akiwa anawachezea ama kuwakera wengine aendelee lakini siyo kwake toto la Malindi.
Mitandao ya kijamii na wengine waliohudhuria mkutano wake wa hadhara wakati akimpasha Atwoli, bado wanangurumwa na mbavu za vicheko alipomtahadharisha Atwoli kwamba “amezoea kupeleka viberiti vya gari (maarufu Probox), je, atawezana na jike dume la Malindi aina ya gari la kifahari la
kisasa aina ya V8?
Kwa wale walio na uzoefu wa tafsiri za masuala ya ndani kama ya Jumwa, ni kumaanisha kwamba alikuwa anamwambia katibu kuwa amezoea kubibinda wafupi lakini hawezani na twiga kama Aisha. Hii ni misemo ambayo inawakera wafuasi wa kila kiongozi anayetajwa lakini kwa kuwa siasa ni karata, huwa hakuna uadui wala chuki isipokuwa ngonjera tu!