Maafisa wa polisi
Uchumi wetu mwafilisi
Wa ufisadi wahandisi
Mwalirejesha nyuma taifa
Polisi wa trafiki
Hakika metudhihaki
Safarini hatufiki
Mwalirejesha nyuma taifa
Vituo vingi barabarani
Vya ufisadi kwa yakini
Noti zakunjwa, zatupwa chini
Mwalirejesha nyuma taifa
Madereva na utingo
Wamechoshwa na hongo
Mewazoesha ndio mtindo
Mwalirejesha nyuma taifa
Maisha ya wasafiri
Yamo kwenye hatari
Hamuyapekui magari
Mwalirejesha nyuma taifa
Mabarabarani mejaa ajali
Mwajibanza na vitambi hamjali
Mepuuza ya barabara hali
Mwalirejesha nyuma taifa
Toshekeni na zenu ajira
Wananchi wamejawa hasira
Mewapunguzia mishahara
Mwalirejesha nyuma taifa
Kasha mwasema mwaonewa
Eti heshima mmekosa kupewa
Tendeni yalo haki na sawa
Mwalirejesha nyuma taifa
Muweni vyombo vya Amani
Wajibikeni mabarabarani
Saidieni kuangamiza ufisadi nchini
Tuiendeleze taifa