Tunaposheherekea leo
Ya mahakama matokeo
Kwa vifijo na nderemo
Wapo walojawa na kilio
READ MORE
Opposition gives Ruto ultimatum over abductions
State defensive as 'missing' Kindiki reappears with New Year posts
Mauaji tulishuhudia
Vifo vingi vilitokea
Mali watu walipoteza
Wapo walojawa na kilio
Ndugu alimgeukia ndugu
Watu wakageuka mapwagu
Nchi ilijawa na vurugu
Wapo walojawa na kilio
Wanawake walibakwa
Makaazi kuteketezwa
Wapendwa waliuawa
Wapo walojawa na kilio
Manyumbani tulihama
Tukaishi kwenye hema
Hatujapata petu pema
Wapo walojawa na kilio
Serikali nayo ahadi
Tele tele iliyoahidi
Hii leo bado miadi
Wapo walojawa na kilio
Ya ICC mahakama
Kwa imani tulitazama
Kesi zote sasa mezima
Wapo walojawa na kilio
Uchaguzi wakaribia
Toafuti twashuhudia
Wa upinzani wajidai
Wapo walojawa na kilio
Kwa kweli twajihadaa
Kwa uchaguzi kuandaa
Bila amani inayotufaa
Wapo walojawa na kilio
Wana machungu mioyoni
Kumbukumbu akilini
Wamekosa haki mahakamani
Wapo walojawa na kilio
Mahakama wameshinda
kwa uweza wa kifedha
mbinguni ni jazanda
wapo walojawa na kilio
twahitaji amani kenya
kabila moja la wakenya
ufisadi tuache Kenya
wapo walojawa na kilio
Hapafai shangilio
Bali mengi maendeleo
Ila serikali ielewe
Wapo walojawa na kilio
©YegonEmmanuel