WIZI
Aibiwa Shilingi Milioni Moja.
Keshia mmoja amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na majambazi waliokuwa na bunduki na kumwibia takribani shilingi milioni moja. Kisa hicho kimetokea katika Mtaa wa Parklands hapa jijini Nairobi. Maafisa wa polisi wanasema keshia huyo alikuwa amechukua fedha hizo kutoka kwenye benki na alipania kuzitumia kuwalipa wafanyakazi wa ujenzi. Hadi sasa hakuna yeyote aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.
Posted on July 29, 2012 na Zubeida Koome
