Uteuzi
Makamishna wa Kaunti; Raila akosoa wizara
Utata unaozingira uteuzi wa makamishna 47 wa kaunti za Kenya umepata umbo jipya. Saa chache baada ya wanaharakati wawili wa haki za binadamu kuwasilisha rufaa kupinga rufaa ya wizara ya usalama wa taifa, Waziri mkuu Raila Odinga ameitaja hatua ya wizara hiyo kuwa potovu. Awali wanaharakati wameitaka mahakam kuu kumchukulia hatua katibu katika wizara ya usalama wa taifa Mutea Iringo kwa kukiuka agizo la mahakama. Wanaharakati hao wanadai kuwa iringo alinukuliwa na vyombo vya habari akiwataka makamishna hao kukaidi agizo la mahakama. Tayari wizara ya usalama wa taifa imepuuza agizo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali Githu Muigai na kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ulitupilia mbali uteuzi wa makamishna wa kaunti
Posted on July 13, 2012 na Sofia Chinyezi
