Gormahia itajitupa dimbani dhidi ya Mathare Ijumaa hii

Na,Hassan Ali

Mechi ya fainali kuwania taji la KPL vijana wasiozidi miaka ishirini imepangiwa kuchezwa Ijumaa hii ambapo Gormahia itajitupa dimbani dhidi ya Mathare. Gormahia imetinga fainali baada ya kuizidia Ushuru mechi ya nusu fainali nayo Mathare ikaibandua Kk Homeboys.