×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Story za mtaa: Ndoa sio mchezo

News
 Ndoa sio mchezo Picha: Hisani

Kuna aina mingi sana za kuoana siku hizi.

Sio kama siku za kitambo wakati kuoana ilikua ni kitu ya kuheshimika. Siku hizi mambo imebadilika kwa sababu ya hii na ile, zamani kuoana haikua mchezo, watu wakioana ilikua ni kwa hiari yao wenyewe.

Walikua wanajuana sana kwanza kabla ya hata kutangaza harusi.

Ndio maana waliooana kitambo wameishi mpaka wa leo wakiwa pamoja na bado wanapendana ni kama walioana jana. Watu wa kitambo wakioana walikua wanajua ni nini wanafanya. Walikua wanajua ukioa ama ukiolewa umefunga pingu ya maisha.

Ndio maana leo nimeamua tubonge na wale watu wanaoana siku hizi juu wanabeba kuoana kama mchezo. Wengi wanasahau kuoana sio mchezo. Siku hizi kuoana imekua ya aina mingi sana juu harusi ziliisha.

Kitambo watu walikua wanafanya mpaka harambee ya harusi ndio watu waoane, wakati huu watu wameleta mchezo juu kuna come we stay, kuna no feelings, kuna kesho kutwa rudi kwenu na zingine mob.

Mnawachana na beste yako leo, kesho ukienda kwake unapata ameoa. Hakuna mtu ameambia ameoa, ama ameolewa. Watu wanaoana tu kwa sababu ya kupigana kuni.

Yaani hakuna mtu ako na feelings na mwenzake, feelings ni saa ya kunyanduana peke yake.

Matotoise wa siku hizi make rada, usidhanie eti kwa sababu unajua kuanika unaweza ukaolewa. Na majamaa mjue kuanikiwa haijafanya ukue qualified kuoa.

Kuoana sio tu eti ni kupigana kuni, kuoana sio mchezo na kuoana ni gharama.

Mkishaoana mkae mkijua nyinyi ni kitu kimoja, msikae mwaka moja mbili ama tatu halafu muanze kuleteana za ovyo.

Pombe ina heshima zake

Pombe sio supu na kila mtu anajua hivyo. Kuna watu wamebeba pombe ni kama supu, hata chakula ikiwa hapo lazima wakunywe pombe kwanza. Wenye shida zaidi ni wale wa pombe ya bure.

Pombe hujanunua, pombe ya kuitiwa na beste yako inabidi unanyonya tei pole pole.

Usikunywe ni kama supu unakunywa. Usiharakishe kutoa lock kuliko mwenye amekuinvite, hata kama ni pombe ya bure, kunywa pole pole usijiabishe juu watu wengi sana hujiabisha kwa pombe za bure.

Unapata mtu anakunywa na fujo mpaka anaanza kutapika kwa event ya wengine na kujiaribia jina. Usikue chupa ya nane na mwenye ananunua ako chupa ya pili, utalewa haraka kabla aitishe crate.

 

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles