×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Maisha Peupe: Je wapenda kazi yako?

News
 Wapenda kazi yako? Picha: Hisani

Katika taaluma yangu ya uwana habari, nimekutana na watu wa tabaka mbali mbali — wakubwa kwa wadogo.

Jambo moja ambalo limejitokeza kila wakati ni jinsi kila mmoja wetu ana ari ya fedha nyingi, maisha mazuri na kadhalika.

Wasilolijua wengi ni kuwa ilikufanikisha ndoto yako — ya kuwa na mambo haya yote — lazima uwe unajihusisha na kazi mmoja au nyingine ili kuishi.

Ndiposa nikaonelea ni vyema nigusie swala la kupenda kazi unayoifanya.

Nimegundua kuwa baadhi ya watu hawapendi kazi zao — wako pale kwa sababu fulani. Kwa mfano waeza kuwa unalipwa mshahara mkubwa, hivyo ikawa sababu ya kufanya kazi.

Vile vile huenda uko pale kwa sababu hauna chaguo lingine ama namna pekee ya kupata riziki.

Sio shaka kuwa watu wengi duniani wamesakamwa ndani ya kazi ambazo hawazipendi hata kidogo, wao wananung’unika kila kuchao. Je, wajua kuwa kazi yako inafaa kuwa kioo cha mwito wako maishani?

Je wajua kuwa kazi unayoifanya lazima ikuridhishe na uipende kwa moyo wako wote? Kazi yako ni kipande cha maisha yako unayoyaishi kila siku? Itakuwaje uchukie kazi za mikono yako?

Hivyo nakuhimiza uwe na ndoto kubwa maishani hata unapojipata unafanya kazi usiyoipenda

Anza kwa kufikiria ni kazi ipi unaweza kufanya na ikakutosheleza. Usidhani kuwa kazi kubwa ni kukaa kwenye ofisi kubwa na kuletewa chai ofisini. Vile vile, kazi mzuri sio ile inayokulipa fedha nyingi mno. Kazi mzuri ni ile itakayokutosheleza.

Kazi itakayokuridhisha ni ile unafanya kwa moyo wako wote na hivyo kuwacha alama ya upendo kwa maisha ya mtu mwingine.

Nishawahi kuwaona kina yaya wanyumbani au hata bawabu ambao wanapenda kazi zao sana — hata wenye kuwaajiri wanawaamini kwa yote.

Hivyo tafuta kazi unayoipenda. Kumbuka unapokuwa katika mazingira ya kazi usiyoipenda, basi mara nyingi unafunga milango ya nguvu na uwezo wako kujidhihirisha wazi kazini. Vile vile unaifungia baraka kazini.

Hebu anza kwa kunena haya: “Kazi yangu inanitosheleza, kwa hali zote, nawasaidia binadamu wenzangu, naelewa mahitaji yao, nafanya kazi na watu wanaonipenda, kazi yangu inanipa uhuru wakujieleza nikiwa kazin, nina furahia na kutosheka na fedha ninazopata kupitia kazi hii.”

Mambo haya yatakusaidia kuleta mafikira yako karibu na maswala kuhusu umuhimu wa kazi unayoifanya kila siku. Kumbuka kuwa kazi yako ni mwito wa maisha yako.

Wasiliana Nami

[email protected]

 

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles