×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Maisha Peupe: Matamshi yako ni hekima kwako

News
 Matamshi yanahitaji hekima. Photo: Courtesy

Je wajua kuwa matamshi au maneno unayotamka kila siku yana nguvu ya kukuangamiza au kukupa buheri maishani mwako!

Hayo ni kweli kabisa na ikiwa haukubaliani nami, basi elewa kuwa hata ulimwengu huu uliumbwa tu kwa maneno, wakati mungu alipoumba dunia alitamka tu maneno na yakawa uhai, vivyo hivyo ndivyo alivyotupa ile nguvu ya kuweza kujitabiria maishani mwetu kulingana na jinsi tunavyowaza rohoni mwetu na akilini mwetu .

Katika maisha haya ambayo nimeishi nimewaona watu ambao hutohoa maneno ambayo yanawadunisha na kuwaweka chini, kwa mfano, iwe ni kwamba unapitia kipindi kizito ukasikia mtu akiyatamka matamshi haya “mimi siwezi kuafikia yeyote” au “mimi ni bure kabisa”.

Je, huoni matamshi haya tayari yamekuangusha chini bila hata kuchapwa na yeyote? Ndiposa leo hii ninapigia debe tabia ya kuweka mafikira yale yanayokunufaisha na kukuendeleza mbele maishani, kwani kilichomoyoni mwako ndicho kitakacho tiririka kutoka kinywani mwako.Iwe vipi basi ukawa unafikiria mawazo yenye kukudunisha na ukatamka vengine ?

Lahasha chochote unachokiwazia leo hicho ndicho utakachotamka lazima uanze kufikiria mambo unayotaka kuyaona maishani mwako kana kwamba yapo , kwa mfano anza kufikiria jinsi ya kuafikia malengo yako na kuwa na mipango ya jinsi ya kuafikia hayo , hebu masikio yako macho yako yakatizama na kusikia yale yenye kunufaisha nafsi yako na maisha yako , kwa kuwa huwezi weka macho yako kwa tunda bovu au kwa watu wenye kuzungumza lugha chafu na ukaendelea kuwa msafi .  

Kuna methali moja inayosema hivi kinga moyo wako kwa kila namna kwani ndani ya chemichemi zake huibua maswala ya maisha yako , hivyo basi wacha moyo wako uwe safi na uwe na fikra nzuri kila wakati livha ya matukio mbalimbali , kwani matamshi yako hayatakuwa mbali na fikra za moyo wako.

 Wasiliana nami

[email protected]

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles