×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Moha Jicho Pevu: Makao makuu ya CID ni jumba la ukabila

News

Kila nikisema taifa la Kenya limebakwa, wachache huniandama na matusi kwa sababu wanajua wanaobaka wakenya ni kina nani.

Kila mara nikisema Kenya yahitaji kiongozi — maana serikali iliyopo imefeli — chuki za kikabila huniandama.

Jameni mwataka nimpake siagi nani ili niridhishe wafuasi wa miungu midogo pamoja na wakabila wao? Leo naelekeza jicho langu ndani ya makao makuu ya CID.

Duru zetu zinatuarifu kuwa idara hii iliyo chini ya Mkurugenzi mkuu wa CID Bw Ndegwa Muhoro imekuwa ikiendeshwa kwa misingi ya kikabila. Hizi ni baadhi ya tetesi kutoka kwa maafisa wadogo wa CID ambao wanahisi ukabila umekithiri katika idara hii muhimu.

Kwa mujibu wao, vyeo na uhamisho hutolewa kwa misingi ya kikabila. Miezi kadhaa iliyopita idara hiyo ya CID ilikashifiwa vikali pale baadhi ya maafisa waliohusika katika uchunguzi wa sakata ya NYS kutajwa kula sahani moja na washukiwa kando, mbali na kutofuata utaratibu unaofaa kwa lengo la kufutilia mbali kesi hiyo.

Mkuu wa kitengo cha upelelezi wa benki Joseph Mugwanja baada ya kutajwa kuhusika katika sakata hiyo, amebakia kuwa mtu huru. Badala ya kusimamishwa kazi kwa muda na kufunguliwa mashtaka, makao makuu ya CID imeanza kucheza shere ili uziba mwanya wa sakata hiyo.

Wakenya wapenda kabila, sasa Joseph Mugwanja, naibu inspekta jenerali wa polisi, amehamishwa hadi Idara ya Polisi Uwanja wa Ndege na mwanya wake kuzibwa na afisa mpelelezi wa kaunti ya Kajiado Ngatia Iregi. Iregi anatajwa na wandani wetu kama kijana wa mkono wa mkurugenzi wa CID Ndegwa Muhoro.

Kwa mujibu wa duru zetu ndani ya idara hii, uhamisho wa Ngatia ni mojawapo ya njia yinayotumiwa na makao makuu ya CID ili kufuta nyayo za sakata ya NYS za mtangulizi wake Mugwanja pamoja na maafisa wengine wakuu.

Ki-madaraka Ngatia Iregi ni afisa mdogo wa polisi. Nafasi alopewa inafaa wapewe maafisa wengine walio na vyeo sawia na Joseph Mugwanja. Swali ni je, ndugu Muhoro anajikinga yeye ama anakinga mtu mwengine? Makao makuu ya CID inadaiwa kujaa uozo wa ukabila. Iwapo umetoka kabila isiyo mamlakani basi wengi wao hujipata kubanwa. Kwa mfano tazama mpangilio huu:

Embu

Afisa mkuu wa CID kaunti ya Embu ni Pius Macharia ambaye wadhifa wake ni ule wa kamishna wa polisi. Alihamishwa kaunti ya Mombasa kabla ya kupelekwa Uingereza kwa miezi kumi kwa mafunzo ya polisi huko Bramshield College. Nafasi yake inashikiliwa kwa muda na Bwana Mugo. Nelson Marwa ndio baba yao. Tizama kwa makini ubabe wa kupigania kura za Mombasa kati ya Upinzani na Jubilee kisha utapata jawabu.

Bonde la Ufa

Gedion Kibunja ndiye kusema na kutenda huko bonde la ufa.

Maafisa wengi wa polisi wanalalamikia utaratibu huo wa kikabila na kusema kuwa iwapo tabia hii itaendelea, basi kutakuwa na shida kubwa ndani ya idara ya polisi kwa jumla.

Nyanza

John Gachomo anaongoza upelelezi wa kaunti ya Nyanza. Wadhifa wake ni ule wa kamishna wa polisi.

Wengine ni Boniface Mwaniki — Garissa — ingawa naarifiwa alidinda kuenda. Henry Ondieki — Nairobi, Francis Macharia — Changamwe, miongoni mwa maafisa wengine wengi.

Makao makuu ya CID

Hili linatajwa kama jumba la dhulma. Kwa sasa anayeongoza uchunguzi wa CID ni John Kariuki. Baadhi ya wakuu wa CID wamebakia na kazi ya kuwakimbiza waandishi wa habari na kuabudu wezi wa ardhi, watapeli wa dhahabu, wizi wa magari na kula sahani moja na mamluki wanaofyonza damu ya wakenya kidhulma.

Vita baridi vinazidi kutanda huku shughuli nyingi za uchunguzi zikizidi kutatizwa. Polisi niliozungumza nao wanadai kuwa iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa basi idara ya polisi itajigawanya mara mbili na kuwa idara ya ukabila na idara ya maafisa waliodhulumiwa, hivyo basi kuwa kama chama cha kisiasa. Tetesi za uchunguzi wao kuingiliwa kati na baadhi ya wakuu wa polisi pia ni mojawapo ya masuala mazito wanayotaka yazungumziwe. Tangu na kuingia mamlakani kwa serikali ya Uhuru Kenyatta na William Ruto, uteuzi wa viongozi umekuwa ukionekana na wengi kama uteuzi wa kulinda kabila zao badala ya kuunda Kenya moja. Polisi na chama cha Jubilee huenda zikawa na sera za kukomboa kabila fulani na kuponda kabila zingine.

Mapema mwaka huu aliyekuwa Naibu Inspekta Jenerali wa polisi Grace Kahindi aliondolewa kidhulma katika ofisi yake na baada ya wapinzani kumtetea Grace Kahindi alifika mahakamani kujitetea zaidi kabla ya mahakama kutoa maamuzi ya nafasi yake kuheshimiwa na kusema maamuzi hayo yalikuwa kinyume na katiba. Hadi wa leo Grace Kahindi anazungushwa mbuyu na wakuu wa polisi wasioheshimu mahakama na katiba ya Kenya.

Siasa za 2017

 Makao makuu ya CID, Nairobi      Picha: Collins Kweyu/Standard

Kwa mtazamo wangu, siasa za mwaka wa 2017 zinaandaliwa kwa misingi ya kuwa na makali ya kutwaa ushindi. Mwaka wa 2007 Mwai Kibaki alitumia maafisa wa utawala kuafikisha malengo yake ya kukalia kiti cha urais. Dalili hiyo sasa inaanza kuonekana tena. Huenda Jubilee inapanga maafisa wakuu wa polisi kikabila ili waweze kuwatumia kuafikisha malengo yao mwaka wa 2017. Letu ni jicho tu zamu ya mengi fiche katika afisi ya Ndegwa Muhoro ikifika tutawajulisha papa hapa.

Mohammed Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN.

Kuwasiliana naye: [email protected], FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali, Instagram: @mohajichopevu, Twitter:@mohajichopevu

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles