Riyad Mahrez Kuhamia Arsenal

Na, Stephen Mukangai

WINGA wa timu ya taifa ya Algeria anayeichezea kilabu ya Leicester City, Riyad Mahrez anawazia kujiunga na timu ya Arsenal. Majarida nchini Ufaransa yamedai kuwa Mahrez amefanya uamuzi wa kuihima Leicester na kujiunga na Arsenal.

MAHREZ mwenye umri wa miaka 25 msimu jana alipachika wavuni magoli 17 na kuisaidia Leicester kulitwa taji la ligi ya BARCLAYS PREMIER kwa mara ya kwanza katika historia. Kufuatia umahiri wake Riyad Mahrez alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika ligi hiyo yenye ushindani mkali.

Inasemekana kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ni shabiki mkubwa wa Mahrez na analenga kuimarisha safu yake ya ushambulizi kwa kumsajili.

WAKALA wa Mahrez alihudhuria mechi ya kirafiki kati Arsenal na Lens nchini Ufaransa na hilo limechochezea uvumi kuwa anaelekea Emirates. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa timu hiyo itatumia pesa nyingi kuimarisha kikosi chake.