Mkenya ataka kuongolewa kwa Moses Kuria kwenye kamati inayojadili suala la IEBC

Huku mchakato wa kutafuta suluhu kuhusu utata ambao umekuwa ukiizingira Tume ya Uchaguzi nchini IEBC ukiendelea, mwanaharakati mmoja amewasilisha kesi mahakamani akitaka kuondolewa kwa Seneta Johnstone Muthama, Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria na mwenzake wa Suna Mashariki Junet Mohamed kwenye kamati ya pamoja ya Jubilee na CORD.
Mwanaharakati huyo, Henry Kioko amesema watatu hao wanakabiliwa na kesi mahakamani kuhusu madai ya uchochezi hivyo hawastahili kuhudumu kwenye kamati hiyo inayotarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu hatma ya makamishna tisa wa IEBC.
Vilevile amesema tajriba ya watatu hao ni ya kutiliwa shaka. Viongozi hao ni miongoni mwa wanane ambao walikamatwa wiki mbili zilizopita kwa tuhuma za kutoa matamshi ya uchochezi.

Na, Beatrice Maganga,

Related Topics