Watu 36 wauliwa katika shambulizi la kigaidi Uturuki

Watu 36 wamefairiki dunia huku wengine 90 wakisalia na majeraha baada ya shambulizi la kigaidi katika Uwanja wa Ndege wa Mataifa wa Ataturk, nchini Uturuki usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, washambulizi watatu waliwavamia rai waliokuwa wakisubiri kuabiri ndege na kuwamiminia risasi. Aidha, magaidi hao walijilipua baada ya polisi kuanza kukabiliana nao. Shambulizi hilo linajiri miezi mitatu tu baada ya wanajeshi watatu kuawa katika shambulizi lingine la  kigaidi nchini humo.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kundi la kigaidi la IS limehusika na shambulizi hilo.

Na,Steve Biko

Aidha, Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan ameongeza kuwa shambulizi hilo litachangia pakubwa mageuzi katika vita vyao dhidi ya ugaidi.

Related Topics