Wanunuzi wa bidhaa watakiwa kuwa makini

Ni sharti wanunuzi wawe makini wakati wa kununua bidha madukani ili kujiepusha na magonjwa. Haya ni kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka la Kukabili Bidha Ghushi Nchini, Anti Counterfeit Agency Agnes Kariu.
Akizungumza jijini Nairobi baada ya kuteketeza bidhaa gushi zenye thamani ya shilingi milioni 58zilizonaswa katika Kaunti za Nairobi, Kisumu, Eldoret na Mombasa, Agnes amesema mamlaka hiyo inaniua kufanya shughuli ya uhamisisho kwa wanunuzi kote nchini.
Aidha amedokeza kuwa tayari walionaswa na bidha hizo wamefunguliwa mashtaka mahakamani.
Baadhi za bidha zilizoteketezwa ni simu za rununu, ala za muziki, vipodozi pamoja na mavazi.

Na, Sulleiman Yeri